// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA WAFIKA SALAMA KIGALI, WAPO MZIGONI KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA WAFIKA SALAMA KIGALI, WAPO MZIGONI KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, February 17, 2012

    SIMBA WAFIKA SALAMA KIGALI, WAPO MZIGONI KESHO

    WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC, wamefika salama mjini Kigali, Rwandea tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya wenyeji Kiyovu Sport.
    Simba waliondoka jana jioni mjini Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda, kuelekea mjini Kigali, Rwanda, tayari kwa mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Jumamosi wiki hii.
    Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange Kaburu amesema leo; "Tumefika salama na tuko tayari kulinda hadhi ya klabu yetu na nchi yetu kwa ujumla, Watanzania watuombee dua,"alisema Kaburu.
    Simba inayofundishwa na Mserbia Milovan Cirkovick, inakwenda Kigali ikiwa katika hali nzuri kimchezo, kwani inaongoza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na katika mechi zake nne za mzunguko huu wa pili, imeshinda tatu na kufungwa moja. Ilizifunga Coastal Union 2-1, JKT Oljoro 2-0 na Azam FC 2-0, wakati yenyewe ilifungwa 1-0 na Villa Squad.   Mwaka jana, Simba ilicheza Ligi ya Mabingwa na katika Raundi ya Kwanza iliitoa Elan Mitsoudje kwa jumla ya mabao 4-2 na Raundi ya Pili ikatolewa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa jumla ya mabao 6-3. Hata hivyo, Simba ilirudishwa na CAF mashindanoni baada ya kushinda rufaa waliyomkatia beki wa Mazembe, Janvier Besala Bokungu, aliyevunja mkataba kinyume cha taratibu na klabu ya Esperance ya Tunisia. Simba ilicheza mechi maalum ya mkondo mmoja na Wydad Casablanca ya Morocco mjini Cairo, kuwania kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa nchini Misri na kufungwa mabao 3-0, hivyo kuangukia kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako ilitolewa na DC Motema Pembe ya DRC kwa mabao 2-1. Simba ndiyo klabu ya Tanzania yenye rekodi nzuri zaidi katika michuano ya Afrika, ikiwa imewahi kufika Fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993, kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003, wakiwatoa wapinzani wa Yanga mwaka huu, Zamalek na pia wakati michuano hiyo ikiitwa Klabu Bingwa Afrika walicheza Nusu Fainali mwaka 1974.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA WAFIKA SALAMA KIGALI, WAPO MZIGONI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top