WAPINZANI wa jadi katika soka ya Uganda, Express 'Tai Mwekundu' na SC Villa 'Jogoo' wametoka sare ya 1-1 katika mechi iliyovikutanisha vikosi vyao vya akiba leo kwenye Uwanja wa Wankuluku.
Katika mechi hiyo ya Ligi ya wachezaji wa akiba Uganda, Derrick Busingye aliifungia bao la kuongoza Express dakika ya 13, kabla ya Ivan Mubiru kuisawazishian Villa kipindi hicho hicho cha kwanza.
Matokeo hayo yanaicha Express katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya rizevu ikiwa na pointi tisa baada ya kucheza mechi sita na Villa ni ya tatu, ikiwa na pointi nane baada ya kucheza mechi sita pia.
0 comments:
Post a Comment