WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC, wanatarajiwa kuondoka leo
saa 11 jioni mjini Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda,
kuelekea mjini Kigali, Rwanda, tayari kuvaana na Kiyovu Sport katika mchezo wa kwanza
wa Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Jumamosi wiki
hii.
Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, amesema leo kwamba maandalizi
yamekamilika.
Alisema wachezaji wote wako katika hali nzuri na wana morali na mchezo huo na wanakwenda kushindana na kurudi na ushindi, ingawa wanaamini mchezo huo utakuwa mgumu kwao kwa kuwa wako ugenini.
Simba inayofundishwa na Mserbia Milovan Cirkovick, inakwenda Kigali ikiwa katika hali nzuri kimchezo, kwani inaongoza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na katika mechi zake nne za mzunguko huu wa pili, imeshinda tatu na kufungwa moja.
Ilizifunga Coastal Union 2-1, JKT Oljoro 2-0 na Azam FC 2-0, wakati yenyewe ilifungwa 1-0 na Villa Squad.
Mwaka jana, Simba ilicheza Ligi ya Mabingwa na katika Raundi ya Kwanza iliitoa Elan Mitsoudje kwa jumla ya mabao 4-2 na Raundi ya Pili ikatolewa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa jumla ya mabao 6-3.
Hata hivyo, Simba ilirudishwa na CAF mashindanoni baada ya kushinda rufaa waliyomkatia beki wa Mazembe, Janvier Besala Bokungu, aliyevunja mkataba kinyume cha taratibu na klabu ya Esperance ya Tunisia.
Simba ilicheza mechi maalum ya mkondo mmoja na Wydad Casablanca ya Morocco mjini Cairo, kuwania kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa nchini Misri na kufungwa mabao 3-0, hivyo kuangukia kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako ilitolewa na DC Motema Pembe ya DRC kwa mabao 2-1.
Simba ndiyo klabu ya Tanzania yenye rekodi nzuri zaidi katika michuano ya Afrika, ikiwa imewahi kufika Fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993, kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003, wakiwatoa wapinzani wa Yanga mwaka huu, Zamalek na pia wakati michuano hiyo ikiitwa Klabu Bingwa Afrika walicheza Nusu Fainali mwaka 1974.

0 comments:
Post a Comment