KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Ramadhan Suleiman Chombo
‘Redondo’ amepata bonge la dini nchini Msumbiji, lakini tatizo anaiogopa klabu
yake Azam, ataianzaje wakati aliitoroka kwenda huko.
Redondo huyo wa Keko, amepata timu Msumbiji na hiyo si
nyingine zaidi ya Ferroviarrio de Maputo, ambayo iko tayari kumpa mshahara wa
dola 1,000 za Kimarekani kwa mwezi na dola nyingine za Kimarekani 9,000 kama
dau la usajili.
Hata hivyo, kitumbua cha mchezaji huyo kipo kwenye hatari ya
kudondokea mchangani kutokana na masharti ya klabu hiyo, inayommiliki na kipa
wa kimataifa nchini, Muharammi Mohamed ‘Shilton’.
Ferroviarrio imemtaka Redondo kwanza awapatie hati yake ya
Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ndipo akabidhiwe dola 9,000.
Lakini kwa sababu Redondo aliondoka kwa kutoroka Azam FC,
anaogopa ataanzaje kuzungumza na viongozi wake, hivyo amebaki Msumbiji tu
anaangalia wenzake wanapocheza.
Habari zaidi ambazo DIMBA imezipata zinasema kwamba, tayari
Azam wamekwishashitukia dili hilo na wamesema hawatamuchia kiungo huyo hadi
wapewe Sh. Milioni 35.
Azam ilitaka kumtoa kwa mkopo Redondo kwenda Villa Squad
Januari mwaka huu, lakini mchezaji huyo akagoma, lakini ajabu timu ilipoingia
kambini hakuonekana tena hadi kuibuka habari yupo Msumbiji.
Kiungo huyo wa zamani wa Simba na Ashanti, aliwahi pia
kutakiwa na harasa El Hodooud ya Misiri mwaka juzi, lakini akaamua kuhamia
Azam.
0 comments:
Post a Comment