MRENO Cristiano Ronaldo alikuwa kinara katika ushindi wa 4-0
wa timu yake, Real Madrid dhidi ya Racing Santander huku yeye akifikisha mabao
28 na kuwaacha wapinzani wao, Barcelona wanaoshika nafasi ya pili kwa pointi 13
katika La Liga.
Ronaldo alifunga bao kwa kichwa dakika ya sita ambalo lilikuwa la 35 anaifungia Real Madrid kwenye mashindano yote msimu huu.
Santander ilicheza pungufu baada ya Domingo Cisma kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 39 kwa kuushika mpira kwa makusudi mara ya pili.
Karim Benzema akapiga mabao dakika ya 45 na 89, katikati ya bao la Angel di Maria, aliyecheza mechi ya kwanza tangu Desemba 17. Barcelona leo wanaikaribisha Valencia inayoshika nafasi ya tatu.

0 comments:
Post a Comment