LONDON, England
KLABU bingwa ya Scotland, Rangers iliyo katika hali mbaya kifedha, imewahakikishia mashabiki wake kwamba itacheza mechi yake ya Jumamosi dhidi ya Kilmarnock.
Wamesema wanafanya jitihadaz a dhati kuhakikisha siku moja tu baada ya kubainika Rangers ni mufilisi, wanasimama imara.
Rangers iko matatani baada ya kubainika inadaiwa kodi dola za KImarekani Milioni 14 katika miezi tisa tu ya timu hiyo kuwa chini ya umiliki wa Craig Whyte.
Uongozi umesema kwamba mashabiki wanahakikishiwa Rangers itaendelea kuwa klabu ya soka . "Lakini klabu imeahirisha tuzo za Hall of Fame katika sherehe za chakula cha usiku zilizopangwa kufanyika Jumapili,"ilisema taarifa ya klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment