WAKATI
kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kiendelea na maandalizi ya mchezo wake
wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ‘The
Leopards’ utakaopigwa keshokutwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, Stars
imepata pigo baada ya nyota wake wawili Juma Jabu na Stephano Mwasyika.
Aidha,
Stars katika mechi hiyo itawakosa nyota wake wawili wanaocheza nje ya nchi,
Nizar Khalfan anayekipiga katika klabu ya Philadelphia Union ya Marekani
na Ally
Badru Ally anayekipiga katika
klabu ya Canal Suez ya Misri.
Mechi hiyo
ni sehemu ya maandalizi ya Stars kuelekea mechi yake ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi
ya Msumbuji ambayo inatarajiwa kupigwa Februari 29 katika Uwanja huohuo.
Ofisa
Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura alisema jana
kwamba Juma Jabu ambaye aliumia na timu yake ya Simba ilipokuwa ikicheza na
Kiyovu ya Rwanda katika mechi ya Shirikisho mwishoni mwa wiki, nafasi yake
itachukuliwa na Waziri Salum wa Azam Fc, huku Mwasyika aliyeumia wakati
akiitumikia timu yake ya Yanga ilipokwaana na Zamalek ya Misri katika ligi ya
Mabingwa Afrika, hali yake inatarajiwa kuimarika ndani ya siku chache.
Aliongeza
kuwa Nizar na Badru hawatocheza mechi hiyo kutokana na kuchelewa kujiunga na
kikosi cha Stars kwani kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la soka Afrika (CAF)
mchezaji anatakiwa afanye mazoezi na timu yake ya Taifa kwa kipindi
kisichopungua siku nne.
Wambura
alisema Stars kuwa kikosi cha Congo kinatarajiwa kuwasili jioni ya leo tayari kwa mchezo huo utakaorindima kuanzia saa 11 jioni.
Kikosi cha
Stars kinachonolewa na Mdenmark, Jan Poulsen kinaundwa na makipa Shabani Kado,
Juma Kaseja na Mwadini Ali, huku mabeki ni nahodha Shadrack Nsajigwa, Masoud
Cholo, Aggrey Morris, Juma Nyoso, Wazir Salum, Stephen Mwasika na Kelvin
Yondani .
Viungo ni Jonas Gerald, Salum Abubakar , Jonas
Gerard, Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Shomari Kapombe, Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, na Abdi
Kassim, huku washambuliaji ni Hussein Javu John Bocco, Nizar Khalfan, Mrisho
Ngasa, Ally Badru Ally, Uhuru Selemani na Nsa Job.
1 comments:
babu kubwa
Post a Comment