KIUNGO wa kimataifa wa Ghana, Sulley Muntari alifunga bao la
kwanza akiwa amevaa jezi ya AC Milan, ambayo iliitandika Cesena mabao 3-1 kwenye
Serie A jana.
Muntari alifunga bao la kuongoza dakika ya 29 kabla ya Urby
Emanuelson kupiga la pili dakika mbili baadaye na Robinho akahitimisha ushidni
huo dakika 10 tangu kuanza kipindi cha pili.
Daniel Pudil aliifungia Cesena la kufutia machozi. Siena ilifungwa 4-1 na Lecce.
Milan sasa inaizidi pointi moja Juventus kileleni, ambayo ina mechi moja mkononi. Timu hiyo mbili zinatarajiwa kukutana wiki ijayo katika mtanange wa kukata na shoka.
Katika mchezo mwingine, Nahodha wa AS Roma, Francesco Totti alicheza mechi ya 700 klabu yake ikishinda 1-0 dhidi ya Parma, kwa bao pekee la Fabio Borini. Lazio ilipigwa 5-1 na Palermo.
Milan iliuatawala mchezo huo na mabingwa hao watetezi walipata bao la kuongoza baada ya Thiago Silva kupiga mpira wa adhabu zambao Francesco Antonioli alishindwa kuuzuia na kumpa fursa Muntari— ambaye amesaini kwa mkopo kutoka Inter Milan mwezi uliopita kufunga kiulaini.
Cesena ilizidi kuporomoka, baada ya Novara, iliyomkia mkiani kutoka sare ya 0-0 na Atalanta. Chievo Verona iliifunga Genoa 1-0 na Udinese ilitoka 0-0 na Cagliari.

0 comments:
Post a Comment