BUENOS AIRES, Argentina
NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi atakiongoza kikosi cha Argentina katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Uswisi Februari 29, mwaka huu.
Kocha wa Argentina, Alejandro Sabella ametaja kikosi chake leo tayari kwa mechi hiyo iloiyo katika kalenda ya FIFA.
Mbali na Messi, kikosi hicho kinawahusisha pia wachezaji nyota kibao wa Argentina, akiwemo kiungo wa Barcelona, Javier Mascherano, mshambuliaji wa Real Madrid, Angel Di Maria na Gonzalo Higuain na mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero.
Carlos Tevez ameachwa kwa sababu hajagusa mpira tangu atibuane na kocha wake Roberto Mancini Septemba, mwaka jana.
Kikosi chenyewe ni hiki, makipa: Sergio Romero (Sampdoria). Mabeki: Hugo Campagnaro (Napoli), Daniel Diaz (Getafe), Federico Fernandez (Napoli), Ezequiel Garay (Benfica), Luciano Monzon (Nice), Marcos Rojo (Spartak Moscow), Pablo Zabaleta (Manchester City). Viungo: Angel Di Maria (Real Madrid), Fernando Gago (Roma), Javier Mascherano (Barcelona), Erik Lamela (Roma), Jose Ernesto Sosa (Metalist), Maxi Rodriguez (Liverpool). Washambuliaji: Gonzalo Higuain (Real Madrid), Lionel Messi (Barcelona), Rodrigo Palacio (Genoa), Sergio Aguero (Manchester City).
0 comments:
Post a Comment