Baadhi ya washiriki wa mbio za kujifurahisha
za”Vodacom 5 KM fun run”wakimaliza mbio zao nakujinyakulia zawadi mbalimbali.
Na Mwandishi Wetu,
Moshi
Mbio za kujifurahisha za kilometa 5 za
(Vodacom 5KM fun run) ambazo ni sehemu ya mbio za Kilimanjaro
marathoni zimezidi kujizolea umaarufu kwa watu wengi wa rika
tofauti kujitokeza kushiriki kwenye mbio hizo zilizofanyika jana/leo mjini Moshi
mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mahusiano wa
kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wa mbio hizo,
Rukia Mtingwa katika mbio za mwaka huu jumla ya watu 10,000 wamejitokeza
kushiriki kwenye mbio hizo tofauti na makadirio ya kawaida ya
kupata jumla ya washiriki 5000 ambacho ndicho huwa kiwango cha juu
.
Mtingwa
alisema wengi wa washiriki katika mbio hizo kwa mwaka huu
zimetokana na uhamasishaji mkubwa uliofanywa na vyombo vya habari na
mvuto wa mbio hizo ambazo huambatana na manjonjo mbalimbali Kutoka
kwa washiriki wake na zawadi za kuvutia zinatolewa na Vodacom.
Pamoja na mafanikio hayo Mtingwa alisema wao kama
wadhamini wamepata changamoto kubwa katika mbio hizo hasa kwa mwaka
huu kutokana na wakimbiaji wazoefu kujitosa kushiriki kwenye mbio
hizo badala ya kuwaachia watu wengine ambao riadha sio fani yao
.
“Kwa kweli mwaka huu tumekumbana na changamoto hiyo ya
wakimbiaji profession kushiriki kwenye fun run ambazo sisi tunaona
ni maalum kwa watu ambao riadhi si fani yao kwahiyo kipindi kijacho endapo
tutaendelea na udhamini wa mbio hizi itabidi tuifanyie kazi changamoto
hii,”alisema Mtingwa .
Aidha Mtingwa alisema changamoto ya kujitokeza
washiriki wengi kwao ni faraja kubwa na watajipanga kukubaliana na
haki hiyo ili kuendana na mazingira ya ukubwa wa mbio
hizo kadiri watu watakavyokuwa wakijitokeza.
Washindi wa mbio za jana/leo kwa upande wa
wanaume ni Gailet Ismail ambaye alichukua na nafasi ya kwanza na
kujinyakulia simu ya mkononi aina ya ZTE S- 501,muda wa maongezi wa Sh 20,000,
modem ya intaneti pamoja na M-Pesa ya Sh 100,000.
Brazil Boay alichukua nafasi ya pili na kuzawadiwa simu
,muda wa maongezi,modem ya intanert na M-Pesa ya Sh 80,000 wakati
mshindi wa tatu alikuwa Fabiano Nelson ambaye naye alipata
simu,muda wa maongezi,modem na M-Pesa ya Sh 60,000.
Na upande wa wanawake washindi walikuwa ni Jackline
Sakilu,Catherine Iranga na Natalia Elisante ambao nao walijishindia zawadi sawa
na zile walizopata wanaume , washindi wengi kuanzia nafasi wanne
hadi 10 pamoja na wshiriki walioweza kumaliza mbio hizo nao walipata zawadi
mbalimbali kutoka Vodacom.
Huo ni mwaka wa tano tokea Vodacom iwe
mdhamini wa mbio za kilometa tano za kujifurahisha (Vodacom fun run)
ambazo ni sehemu ya mbio maarufu za Kilimanjaro ambazo mwaka huu zimeadhimisha
miaka 10 tokea kuanzishwa kwake .
0 comments:
Post a Comment