Katika juhudi za kuwaenzi wanamichezo walioliletea sifa kubwa
taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) iko kwenye mchakato wa kuanzisha
Taasisi ya Michezo ya Rashid Matumla (Rashid Matumla
Sports Academy )
ya kuibua vipaji vya vijana wanaochipukia katika michezo hususan ngumi.
Huu ni mkakati wa kumwandaa bingwa wa zamani wa dunia
aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (Rashid Matumla) kustaafu ngumi ili
aweze kutumia kipaji chake cha ngumi kuendeleza vijana.
TPBC inajivunia historia nzuri ya Rashid Matumla kwa kuwa bondia
wa kwanza Tanzania
kuwa bingwa wa dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (WBU) pamoja na
sifa kemkem alizoliletea taifa hili kipindi hiki chote anachopigana ngumi. Tunapenda kuutangazia umma kuwa
tunamwandalia Rashid Matumla mazingira mazuri ya kustaafu ngumi.
Katika
taasisi hiyo ya Rashid Matumla Sports Academy, Rashid atakuwa ndiye Rais na
atakuwa analipwa mshahara kama mwajiriwa kwa kipindi chote cha uhai wa taasisi
hiyo na kumfanya aweze kujipatia ajira ya kudumu wakati hachezi tena ngumi. Huu
ni moja ya mikakati ya TPBC kuhakikisha kuwa mabondia wake walioiletea nchi hii
heshima kubwa wanaenziwa kwa kuandaliwa maisha mazuri wanapostaafu ngumi!
Ni lazima
kama taifa tuwajali wale wote wanaolipigania taifa hili na tutaendelea pia
kuandaa mazingira mengine ya kuwawezesha waishi vizuri na kuheshimiwa daina ili
kuleta changamoto kwa wengine ili nao wapigane kufa na kupona kuliletea sifa
taifa letu katika michezo.
Taasisi hii
itazinduliwa rasmi wakati wa mpambano wa Rashid Matumla na Vitaly Shemetov
bondia anayetoka Urusi litakalofanyika mjini Moshi tarehe 22nd Juni na
kuhudhuriwa na Mcheza sinema maarufu wa Marekani, Deidre Lorenz wa sinema
maarufu ya Santorini Blue. Mcheza sinema huyo atakuwepo nchini kwa ajili ya
kukimbia mbio za Marie Frances Mt. Kilimanjaro Marathon kusheherekea miaka 50
ya uhuru wa Tanganyika zikazofanyika tarehe 24 Juni mwaka huu kuanzia Moshi
Club.
Taasisi ya
Rashid Matumla Sports Academy ambayo itakuwa inafanya kazi nchi nzima
itajumuisha pia bingwa mwingine wa zamani wa dunia aliyetambuliwa na Umoja wa
Ngumi wa Dunia (WBU) Magoma Shaban. Hawa wote watakuwa waajiriwa wa taasisi ya
Rashid Matumla Sports Academy wakifanya kazi za kuibua vipaji kwa vijana
Tanzania nzima!
0 comments:
Post a Comment