KLABU ya Marseille imefuzu kuingia Robo Fainali ya Kombe la Ufaransa, baada ya kuitandika Bourg-Peronnas mabao 3-1 usiku wa jana, wakati bao pekee la Nene liliibeba Paris Saint-Germain pia hadi hatua hiyo ya michuano hiyo. PSG iliifunga Dijon 1-0.
Mabao ya Marseille yalifungwa na Brandao dakika ya 28 na 45 na kinda wa Ghana Jordan Ayew dakika ya 54, wakati la kufutia machozi la wapinzani wao lilifungwa na Ousmane Diaby dakika ya 78. Kiungo Mbrazil, Nene aliibeba PSG kwa bao lake pekee dakika ya 15.
0 comments:
Post a Comment