'MUUWAJI' Sergio Aguero aligonga vichwa
vya habari wakati Manchester City ilipothibitisha ni bora zaidi kwa
kuilaza Porto magoli mengi na kuwa miongoni mwa timu 16 ambazo zimesalia
kwa hatua itakayofuata ya ligi ya Europa, wakati Jumatano jioni
ilipowafunga 4-0 (kwa jumla 6-1).
Mchezaji huyo wa Argentina alipata bao la kwanza
dhidi ya mabingwa watetezi Porto baada ya sekunde 19 tu kwa mpira wa
chini kwa chini.Kisha alimsaidia mwenzake Edin Dzeko kufunga bao ambalo lilimkasirisha mchezaji wa Porto, Rolando, na kufuatia malalamiko yake, mwamuzi alimuamuru kuondoka uwanjani.
City walitambua udhaifu wa Porto, na David Silva na mchezaji wa zamu David Pizzaro wakaongezea mabao mawili zaidi.
Ushindi huo, ingawa kifedha hauwezi kuziba pengo la kuondolewa mapema pasipo kuvuka hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, angalau utawatuliza City kidogo.
Manchester City kwa hivi sasa hawajishindwa katika mechi 16 za Ulaya wakicheza katika uwanja wa nyumbani, katika kipindi kuanzia tarehe 14 Agosti 2008, waliposhindwa 1-0 na FC Midtjylland katika mechi ya kombe la Uefa.
0 comments:
Post a Comment