KLABU ya Manchester City imewasilisha malalamiko rasmi Shirikisho la Soka Ulaya (UEAFA), ikilalamikia baadhi ya wachezaji wake kufanyiwa kejeli za kibaguzi katika mechi ya Europa League dhidi ya Porto.
City ilishinda 2-1 kwenye Uwanja wa ugenini wa
Estadio do Drago, lakini baada ya mechi hiyo klabu hiyo ilisema kwamba Mario Balotelli
alifanyiwa kejeli za kibaguzi kutoka jukwaani. Mchezaji nmwenzake, Yaya Toure alisema: "Niloisikia kitu fulani.
"Hii, ndiyo maana tunapenda Ligi Kuu (England), hayatokei mambo kama haya huko. Labda nchi nyingine hazitarajii wachezaji weusi."
Waandaaji wa michuano hiyo, UEFA wamesema walikuwa bado wanasubiri taarifa rasmi kutoka kwa maofisa wao, ambayo kwa kawaida hufika siku moja au mbili baada ya kila mechi na baada ya hapo wataipitia na kuchukua hatua.
0 comments:
Post a Comment