// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LIGI DARAJA LA KWANZA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LIGI DARAJA LA KWANZA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, February 17, 2012

    LIGI DARAJA LA KWANZA

    LIGI Daraja la Kwanza Tanzania Bara, (FDL) inaendelea wikiendi hii ambapo kesho (Februari 18 mwaka huu) kutakuwa na mechi ya Kundi C kati ya Polisi Morogoro na Rhino FC ya Tabora itakayochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
    Keshokutwa (Februari 19 mwaka huu) Kundi A ni kati ya Morani FC na Temeke United zitacheza mkoani Manyara na Februari 20 mwaka huu ni Transit Camp na Polisi Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Burkina Faso na Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Jamhuri.
     Kundi B Februari 19 mwaka huu Small Kids itaikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Mlale na Polisi Iringa kwenye Uwanja wa Majimaji na Tanzania Prisons na Majimaji kwenye Uwanja wa Sokoine.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIGI DARAJA LA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top