// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KUMEKUCHA KILI MARATHON 2012 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KUMEKUCHA KILI MARATHON 2012 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 16, 2012

    KUMEKUCHA KILI MARATHON 2012

    WANARIADHA nyota wa ndani na nje ya nchi wamethibitisha kushiriki katika mbio za Kilimanjaro Marathon kwa mwaka 2012 zitakazofanyika Februari 26 mwaka huu. 
    Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Julius Msomi alisema kuwa mwaka huu mbio hizo zitaenda sambamba na mafunzo maalumu kwa wanariadha watakaoshiriki. 
    Aliwataja baadhi ya wanariadha hao kuwa ni Andrea Silvini, Daudi Joseph, Getuli Bayo na Kagera Humay ambao wataungana na wanariadha wanaume kuchuana katika mbio za kilometa 42.195. 
    Aliwataja wanariadha maarufu wengine kuwa ni Fabian Joseph, Damian Chopa, Faustine Musa na Mary Naali watachuana katika mbio za nusu Marathon ambazo zitaanzia katika uwanja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS). 
    Alifafanua sifa za baadhi ya wanariadha wanaoshiriki kwa kusema kuwa wengi wao wana sifa za kimataifa huku wakiwa wameshinda mashindano mbalimbali yaliyowahi kufanyika ndani ya nchi.
    Alisema kuwa wanariadha wanaume ni wale wenye uwezo wa kufika mstari wa mwisho kwa muda usiozidi saa mbili na dakika kumi huku wanawake wenye uwezo wa kufika mstari wa mwisho chini ya saa mbili na nusu. 
    Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Wild Frontiers inayoandaa mashindano hayo alisema kuwa mwaka huu wakimbiaji 5,000 kutoka mataifa 40 ya mabara sita wanatarajia kushiriki mashindano hayo. 
    Pia watu wenye aina mbalimbali ya ulemavu nao watapata nafasi ya kushindana kupitia mbio za nusu Marathon huku kesho ikiwa ni siku ya mwisho kujisajili katika mtandao wa mbio hizo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KUMEKUCHA KILI MARATHON 2012 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top