KLABU ya Juventus ilirejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Italia,
Serie A kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Catania.
Pablo Barrientos aliwafungia wageni bao la kuongoza dakika ya nne, lakini Andrea Pirlo akasawazisha dakika ya 22.
Marco Motta anayecheza kwa mkopo Catania kutoka Juventus tangu Januari, alipewa kadi ya pili ya njano dakika ya 65 na Giorgio Chiellini akaifungia la pili Juve dakika ya 74 kabla ya Fabio Quagliarella kupiga la tatu dakiika ya 80.
Juventus wasiofungika, sasa wana pointi 49, mbili zaidi dhidi ya mabingwa watetezi AC Milan, ambao leo wanacheza na Cesena. Milan itakutana na Juventus Februari 25.

0 comments:
Post a Comment