MSHAMBULIAJI Klaas-Jan Huntelaar alifunga mabao mawili na
kuisaidia Schalke kuilaza Wolfsburg mabao 4-0 katika Bundesliga jana.
Huntelaar pia alipiga penalti iliyookolewa na kipa wa Wolfsburg,
Diego Benaglio. Huntelaar sasa analingana na Mario Gomez wa Bayern Munich kwa
mabao, kila mmoja 18 na Schalke inaongoza Bundesliga kwa jumla ya mabao 50.
Hannover iliifunga Stuttgart 4-2, Christian Pander akifunga moja na kupika mawili.
Borussia Dortmund inaongoza ligi hiyo ikiizidi pointi tatu Borussia Moenchengladbach.
Hannover iliifunga Stuttgart 4-2, Christian Pander akifunga moja na kupika mawili.
Borussia Dortmund inaongoza ligi hiyo ikiizidi pointi tatu Borussia Moenchengladbach.
0 comments:
Post a Comment