RAIS wa
bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ Nyoshi El Saadat
anatarajiwa kurejea nchini Ijumaa
akitokea nchini Uholanzi alipokwenda kuzifanyia ‘Mastering’ nyimbo zao nne ambazo zitakuwemo
kwenye albamu yao mpya zitakazokuwemo kwenye albamu yao mpya inayokwenda kwa
jina la 'Chuki ya Nini' na kuzitaja nyimbo hizo ni pamoja na Otilia, Ndoa ya Kisasa, Dai Chako Ulaumiwe na
Fataki.
Mara baada ya kuwasili siku hiyo atahudhuria
onyesho la bendi hiyo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho,
uliopo Kijitonyama jijini dar es Salaam
ambalo litakuwa mahususi kwa ajili ya kumkaribisha.
“Nawaomba mashabiki wa FM Academia
mjitokeze kwa wingi siku hiyo katika ukumbi wetu pale Makumbusho kwani pamoja
na burudani toka kwa bendi yenu pia nitakuja na mazawadi kutoka Uholanzi ambayo
yote ni sehemu ya kuwapa raha,”Alisema.
0 comments:
Post a Comment