MWANASOKA bora wa zamani wa dunia, Ronaldinho na Vagner Love
walifunga mabao kipindi cha pili na kuisaidia Flamengo kutoka nyuma na kuibuka
na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Resende jana katika Nusu Fainali ya Guanabara
Cup, hatua ya kwanza ya Rio championship.
Vasco da Gama, Botafogo na Fluminense pia zimeingia Nusu
Fainali.
Flamengo ilitanguliwa wakati Marcelo Regis alipoifungia Resende dakika ya 47, lakini Ronaldinho na mshambuliaji wa zamani wa CSKA Moscow, Vagner Love wakaifungia klabu hiyo maarufu zaidi Brazil dakika 10 baadaye, wakipishana dakika tano tano.
Ronaldinho alisawazisha kwa kichwa dakika ya 57 na Vagner Love aliyesajiliwa hivi karibuni, akapiga la pili dakika ya 62. Mshambuliaji Negueba alihitimisha ushindi kwa bao lake dakika ya 72.
Matokeo hayo yatawakutanisha na na Vasco da Gama katika Nusu Fainali, ambayo iliifunga Boavista 1-0.

0 comments:
Post a Comment