BONDIA Muingereza, mzaliwa wa Zimbabwe, Dereck Chisora amemzaba kofi mpinzani wake Vitali Klistchko kabla ya pambano lao la mjini Munich, Ujerumani usiku wa leo.
Ripoti zasema Chisora alimrushia kofi Klitschko, ambaye ni bingwa mtetezi wa masumbwi ya uzito wa juu WBC, katika Mkutano na Waandishi wa Habari baada ya wote wawili kupimwa uzito, tayari kwa pambano la mjini Munich, Ujerumani. Klitschko, ambaye ni raia wa Ukraine, alijizuia kujibu kofi hilo na kukitaja kitendo cha Chisora kama cha kustajabisha.
Chisora, mwenye umri wa miaka 28, amesema licha ya kukosa uzoefu, atampokonya Klitschko taji lake.
Kwa upande wake, Klitschko amejigamba kwamba hakuna wa kumbabaisha katika harakati za kutetea ubingwa wake.
0 comments:
Post a Comment