MASHETANI WEKUNDU, Manchester United jana waliponea chupuchupu kutolewa na Ajax ya Uholanzi katika Europa League kwenye Uwanja wa nyumbani, Old Trafford.
Licha ya hofu iliyosababishwa na Ajax, Man United ilifuzu kuwa miongoni mwa vilabu 16 ambavyo vitaendelea kucheza katika ligi hiyo ya Europa.
Sasa Man U inatazamiwa kukutana na Athletic Bilbao ya Uhispania
Lakini kutokana na wingi wa mabao, Man U ilifuzu kwa jumla ya magoli 3-2.
Ajax awali ilikuwa imeangamizwa kwa bao la awali la Javier Hernandez, baada ya kugongewa mpira vyema na Dimitar Berbatov.
Ingawa Man U wako njiani kuelekea kwa fainali Bucharest, ambako fainali itafanyika, kushindwa kwa timu hiyo kuliondoa matazamio mengi ya mashabiki, baada ya meneja wa muda wa timu ya England, Stuart Pearce, kuwachagua wachezaji sita kutoka Old Trafford, na ambao ni miongoni mwa wachezaji 25 watakaopambana na Uholanzi, Jumatano ijayo, katika mechi ya kirafiki.
Pearce alikuwepo uwanjani kutizama namna wachezaji wanne, kati ya hao sita, wakicheza; Tom Cleverley, Chris Smalling, Ashley Young na Phil Jones.
Licha ya kwamba Man U ilikuwa imeishinda Ajax, mabingwa mara nne barani Ulaya, walipokutana katika mechi yao ya awali, meneja Sir Alex Ferguson hakutaka utani katika mechi ya Alhamisi.
0 comments:
Post a Comment