AZAM FC jana jioni iliifunga Villa Squad mabao 4-1 katika mchezo wa 18 wa ligi kuu ya Vodacom ambayo sasa imebaki wastani wa michezi nane.
Villa Squad ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli lililofungwa na Nsa job katika dakika ya 18 lakini Salum Abubakar alisawazisha kabla ya Abdi kassim Babi kuongeza la pili
Azam FC ilipata goli la tatu kupitia kwa Khamis Mcha khamis Viali kabla ya Kipre Tchetche hajafunga la nne muda mchache kabla ya mapumziko.
Azam FC iliingia kipindi cha pili ikiwa na lengo la kulinda ushindi wake ambapo ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Abdi Kassim na kuingia Jabir Aziz, Kipre Tchetche alimpisha Samih Haji Nuhu na Khamis Mche akampisha Zahoro Pazi.
Kesho ni mapumziko na Azam FC itarejea tena mazoezini keshokutwa
Azam FC; Mwadini Ally, Shikanda, Waziri Salum, Luckson Kakolaki, Erasto Nyoni, Kipre Bolou, Kipre TChetche, Salum Abubakar, Gaudence Mwaikimba, Abdi Kassim na Khamis Mcha Khamis.
0 comments:
Post a Comment