TANGU imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga ya Dar es Salaam haijawahi kushinda mechi, jambo ambalo linachukuliwa kama inacheza ili kukamilisha ratiba tu.
Ilijihakikishia ubingwa baada ya kuifunga Toto Afrika mjini Mwanza na kutimiza pointi 46, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, wakati katika mechi iliyofuata ilitoa zawadi ya pointi moja kwa Kagera Sugar inayopigania nafasi ya pili, kabla ya kuwapa pointi zote tatu Azam FC waliozihitaji ili kujihakikishia kubaki Ligi Kuu msimu ujao. Yanga ambayo baada ya kuilaza Toto 2-1 mjini Mwanza ilikwenda kulazimishwa sare ya 1-1 na Kagera nyumbani, Dar es Salaam kabla ya kufungwa 3-2 na Azam, kesho inamenyana na Polisi Dodoma inayopigana kuepuka balaa la kushuka daraja.
Wachezaji watano tegemeo wa Yanga, ambvao Aprili 19, mwaka huu itamenyana na watani wao wa jadi, Simba wamebaki Dar es Salaam, kutokana na kuwa majeruhi.
Hao ni mabeki Nsajigwa Shadrack, Hamisi Yussuf, George Owino na kiungo Amir Maftah.Je, Yanga itaamua kufanya kweli kesho au itaendelea kugawa pointi? bongostaz inasubiri kuona mambo yatakuwaje hapo kesho. (Pichani kushoto ni kipa anayetarajiwa kudaka leo, Juma Kaseja)
0 comments:
Post a Comment