KIPA aliyedaka katika mechi ya Yanga dhidi ya watani wao wa jadi, Simba Mserbia Obren Curkovic hivi sasa yuko kwao Serbia kabla ya kwenda Austria kufanya majaribio ya kucheza soka hya kulipwa huko.Kuondoka kwa kipa huyo ina maana sasa Yanga imebakiwa na makipa wawili tu, Juma Kaseja na Steven Malashi aliyesajiliwa kutoka kikosi cha pili.
Aprili 19, mwaka huu Yanga itakuwa na mtihani mgumu mbele ya watani wake hao tena, Simba ambao watapigana kufa na kupona ili washinde mechi hiyo na kupata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba inaitaka nafasi hiyo kwa udi na uvumba ili iiwakilishe nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya mwaka huu kuwa benchi wakizishuhudia Yanga na Prisons zikifanya vkitu vyao.
Bila shaka, Juma Kaseja ndiye anayepewa asilimia kubwa ya kuwa langoni siku hiyo, kipa huyo aliyeidakia Simba tangu mwaka 2002 kabla ya kuhamia Yanga mwaka jana, hakika ndiye aliyebeba matumaini ya wana Jangwani kwa sasa kuelekea kwenye mchezo huo.
Je, ataweza kusimama langoni kwa dakika 90 bila kuruhusu bao kama ilivyokuwa kwa Obren Oktoba 26 mwaka jana, wakati bao pekee la Ben Mwalala linaipa Yanga ushindi wa 1-0?
Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona, lakini dhahiri kiu ya Yanga ni kurudia kuifunga Simba Aprili 19, ili wadhihirishe kwamba hawakubahatisha Oktoba 26, mwaka jana na sasa wamefuta kabisa uteja wao kwa watani wao hao wa jadi, ambao wamekuwa wakiwafunga mfululizo tangu mwaka 2004. bongostaz tunasema tunasubiri wakati ufike tuone mambo yatakuwaje siku hiyo.
0 comments:
Post a Comment