KUTOKANA na kauli mbiu ya kumtafuta Miss Tanzania mwaka huu kulenga sekta ya utalii, Mratibu wa Mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga amewataka mawakala kuwahamasisha wananchi kuwa na tabia ya kutembelea maeneo ya vivutio.
Akizungumza jana, Lundenga alisema mawakala hao inawabidi kuwa wabunifu wa kugundua sehemu muhimu ambazo ni za asili na wananchi wamezisahau kufanya matembezi na kugundua nini asili ya sehemu fulani.
Alisema:"Mtanzania wa sasa atashindwa kueleza asili ya nchi yake kwa kutokufahamu maeneo yenye vivutio na hata maeneo ya asili ikiwemo hifadhi za kale."
Akizitolea mifano sehemu za kiasili kama maeneo ya kihistoria Watanzania watenbelee na hii pia itasaidia kukuza uchumi wa Watanzania wenyewe na si kusubiri wageni.
Alisema mawakala hao inabidi wawe na ushirikiano na mamlaka husika kama mbuga za wanyama na wanapokwenda waongee na wakuu wa Mikoa na Wilaya watembelea sehemu za vivutio hivyo wasiwe wavivu na wapeleke taarifa na mipango yao kwa kutangaza utalii kwa jamii. Mawakala hao walichaguliwa kutoka mikoa na kanda mbalimbali wapao 30 na kupatiwa semina ya siku mbili kuhusiana na utalii pamoja na masuala ya urembo.

0 comments:
Post a Comment