// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TENGA AWATAKA MAKOCHA WAZALENDO WAMSAIDIE MAXIMO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TENGA AWATAKA MAKOCHA WAZALENDO WAMSAIDIE MAXIMO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, March 03, 2009

    TENGA AWATAKA MAKOCHA WAZALENDO WAMSAIDIE MAXIMO

    RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Leodgar Tenga, amewataka makocha wa Tanzania, kumsaidia kocha Mkuu wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, Mbrazil Marcio Maximo (PICHANI JUU).
    Tenga ameyasema hayo katika ufunguzi wa semina ya makocha iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na kuratibiwa na Chama Cha Makocha Tanzania (TAFCA).
    Akizungumza katika ufunguzi huo, Tenga alisema kumsaidia huko kutatokana na mafanikio ya semina iliyoandaliwa na CAF na kuhakikisha kwamba kwenye vilabu vyao kunatoa wachezaji bora watakaoitwa na Maximo.
    Alisema wachezaji imara watatoka kwenye vilabu imara, wanaofundishwa na makocha wenye ujuzi katika kiwango cha soka na kuing’arisha nchi katika soka la Kimataifa.
    “Nawataka makocha wote mliopata bahati ya kuitwa kwenye semina hii, muhakikishe kwamba mnakwenda kutoa wachezaji wazuri katika timu zenu na kumpa urahisi kocha wa Stars, Marcio Maximo,” alisema.
    “Huu ni muda wa kung’ara Kimataifa katika nyanja ya soka, lakini naona endapo mtazingatia katika mafunzo haya, nchi itapiga hatua kubwa na kujitangaza zaidi kuwa na sisi tunaweza kucheza soka,”
    Semina hiyo iliyoanza jana jijini Dar es Salaam, inatarajiwa kufungwa Machi Nane mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TENGA AWATAKA MAKOCHA WAZALENDO WAMSAIDIE MAXIMO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top