// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MWALALA AMPA '5' MJERUMANI HARAMBEE STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MWALALA AMPA '5' MJERUMANI HARAMBEE STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 02, 2009

    MWALALA AMPA '5' MJERUMANI HARAMBEE STARS



    MSHAMBULIAJI wa kulipwa wa Yanga kutoka Kenya, Benard Mwalala( wa pili kutoka kushoto pichani), amesema amefurahishwa na kitendo cha kocha mpya wa timu ya soka ya taifa ya nchi hiyo, Harambee Stars, Mjerumani Antoine Hey, kumwita katika kikosi hicho na kukamilisha malengo yake ya muda mrefu.
    Mwalala ambaye aliwahi kuichezea Harambee Stars miaka ya nyuma na baadae kutemwa, amerejeshwa katika kikosi ambacho kinachojiandaa na raundi ya pili ya michuano ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini na Mataifa ya Afrika mwaka huo, nchini Angola.
    Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwalala alisema kwamba siku zote akiwa anaichezea klabu yake ya Yanga, amekuwa akijitahidi ili aweze kupata nafasi ya kurudishwa katika timu ya taifa kwa uwezo na ubora wa soka lake jambo ambalo amefanikiwa na kutimiza lengo lake.
    “Kwa kweli nimepokea kwa furaha taarifa hiyo ambayo kwa siku zote wakati naichezea Yanga nilikuwa nikiamini kwamba ipo siku nitarudi katika timu ya taifa kutokana na juhudi zangu ambazo tayari zimeonekana,” alisema.
    Alisema pamoja na kuitwa katika kikosi cha Harambee Stars hawezi kubweteka kwani ataendelea kujituma zaidi kwa kuwa anaamini timu hiyo itaweza kufika mbali katika michuano hiyo maarufu katika soka duniani ambayo ataitumia kwa ajili ya kutafuta soko la nje kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa.
    Kiwango cha Mwalala kimezidi kupanda akiwa Yanga hasa timu hiyo ya Jangwani ilipomsajili mshambuliaji mwingine wa kulipwa kutoka katika nchi hiyo, Boniface Ambani, ambaye anaongoza kwa ufungaji wa mabao katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ipo katika mzunguko wa pili.
    Mwalala alisema Harambee Stars itaweza kufika mbali kwa kufanya vizuri katika michuano hiyo ya kufuzu Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika na zaidi itatumia nafasi katika mechi zake ambazo itakuwa ikicheza nyumbani.
    Katika michuano hiyo, Harambee Stars imepangwa katika kundi moja na timu nyingine za Nigeria, Tunisia na Msumbuji ambazo hata hivyo mshambuliaji huyo amesema timu zote zina upinzani kwa kuwa hakuna timu inayotabirika katika mchezo wa soka.
    Harambee Stars inatarajiwa kuanza mazoezi rasmi leo ikiwa chini ya kocha huyo mpya ambaye amedai anahitaji kuwaona wachezaji wote aliowaita katika kikosi hicho wakiwemo mlinzi wa Yanga George Owino, Ambani na Mwalala.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWALALA AMPA '5' MJERUMANI HARAMBEE STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top