NI Mussa Hassan Mgosi pekee katika wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars walioshiriki Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), aliyeingia kwenye kikosi cha kombaini ya michuano hiyo, tena kama mchezaji wa akiba.
Katika michuano hiyo iliyomalizika jana kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutwaa ubingwa baada ya kuifunga, Ghana 2-0, Tanzania ilitolewa Raundi ya Kwanza kwenye kundi lake A, ambalo Zambia na Senegal zilizonga mbele.
Mshambuliajiwa DRC, Tresor Mputu Mabi anayewaniwa na Arsenal ya England, ndiye aliyechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa fainali hizo, wakati mshambuliaji wa Zambia, Given Singuluma aliibuka mfungaji bora wa CHAN ya kwanza kutoka na kufunga mabao matano.
Michuano hii ilishirikisha wachezaji wanaocheza Ligi za nyumbani kwao pekee na DRC mbali na kutwaa ubingwa, pia ilitwaa tuzo ya kucheza soka ya kiungwana uwanjani, Fair Play.
Kikosi cha CHAN ni; Mamadou Ba (Senegal), Samuel Inkoom (Ghana), Ofusu Appiah (Ghana), Gladys Bokese (Drc), Harrison Afful (Ghana), Jonas Sakuwaha (Zambia), Kazembe Mihayo (Drc), Bongeli Lofo (Drc), Given Singuluma (Zambia), Tresor Mabi Mputu (Drc) Na Moustapha Diallo (Senegal).
Wachezaji Wa Akina Ni Kipa Samir Abud (Libya), Ovidy Karuru (Zimbabwe), Mussa Mgosi (Tanzania), Ibrahim Ayew (Ghana), Mamadou Baila Traore (Senegal) Na Charles Asampong Taylor (Ghana).
Katika michuano hiyo Stars iliambulia kutikisa nyavu mara mbili kupitia kwa Mrisho Ngassa wakati inaibuka na ushindi wa 1-0 dh9idi ya wenyeji Ivory Coast na Shadrack Nsajigwa aliyefunga kwa penalti dhidi ya Zambia wakati zinatoka sare ya 1-1.
0 comments:
Post a Comment