// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KONDIC AMPOKEA KWA SHANGWE OWINO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KONDIC AMPOKEA KWA SHANGWE OWINO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 01, 2009

    KONDIC AMPOKEA KWA SHANGWE OWINO


    KUREJEA kwa kiungo wa ulinzi wa Yanga, Mkenya George Owino(anayeambaa na mpira pichani) , kumempa faraja kubwa kocha wa kikosi hicho, Dusan Kondic katika maandalizi yake ya mechi ijayo ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri katikati ya mwezi huu.
    Akizungumza wakati wa mazoezi ya timu hiyo katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, mjini Dar es Salaa, alisema ujio wa kiungo huyo unamuongezea imani ya kufanya vizuri katika mchezo huo.
    Owino alikuwa kwao Kenya, kuhudhuria msiba wa baba yake mzazi na hakushiriki hata raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Etoile d’O’r Minorsty ya Comoro, wakati Yanga ilipofuzu ushindi wa jumla wa mabao 14-1.



    MFUNGAJI BORA LIGI YA VIJANA
    KUPANDISHWA AZAM YA WAKUBWA

    WACHEZAJI nyota wa Azam FC Kheri Habib na Sino Agustino wa timu ya soka ya vijana, juzi walipendekezwa kuwamo katika kikosi cha timu ya wakubwa kinachoshiriki Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.
    Akizungumza mara baada ya fainali iliyofanyika juzi katika uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam na timu hiyo kuibuka bingwa kwa kuicharaza Villa Squad mabao 2-0, kocha wa Azam FC, Mbrazil Itamar Amorin alisema kwamba wachezaji hao wameonesha uwezo mzuri na kuwa watawajenga zaidi ili waweze kucheza Ligi Kuu.
    Alisema kwamba lengo la timu yao ya vijana ni kulea vipaji na kuvitumia katika timu ya wakubwa, hivyo hakuna sababu ya kuwaacha wachezaji hao baada ya kuonyesha kiango cha kikubwa katika michuano hiyo.
    Habib ndiye aliyeibuka mfungajibora kwenye michuano hiyo ambayo makinda ya vigogo, Simba na Yanga yalingo’olewa mapema baada kuzifumania nyavu mara sita.
    Michuano hiyo iliyoshirikisha klabu 11 za vijana kutoka klabu za Ligi Kuu baada ya Kagera Sugar pekee kushindwa kuleta yosso wao mjini Dar es Salaam, iliandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na ilianza Februari 14, mwaka huu, chini ya udhamini wa Bakhresa Food Product, kupitia maji ya Uhai.


    KIPINGU AIMWAGIA PONGEZI TFF


    MWENYEKITI wa Baraza la Michezo nchini(BMT),Idd Kipingu,amelipongeza Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kwa kuweza kuandaa Ligi Kuu ya soka Bara kwa timu za vijana na kuwataka waboreshe zaidi michuano hiyo ili kukuza mchezo huo nchini.
    Akizungumza mjini Dar es Salaam juzi mara baada ya fainali kati ya Villa Squad na Azam FC iliyoibuka bingwa wa michuano hiyo, alisema kwamba ni jambo zuri na la kipekee kuanzisha michuano hiyo ambayo inatoa ishara nzuri kwa maendeleo ya soka nchini.
    Kipingu alisema pia anawashukuru wadhamini wa michuano hiyo, Kampuni ya Bakhresa Food Product kupitia maji ya Uhai kwa kujitolea kwao kuibeba Ligi ya vijana ikiwa ni pamoja na kutoa zawadi kwa washindi, kwani huo ni mwanzo na anaamini mwakani michuano hiyo itakuwa bora zaidi.
    Mwenyekiti huyo wa zamani wa TFF, ilipokuwa ikiitwa FAT (Chama cha Soka Tanzania, ametoa wito kwa makampuni na mashirika mbalimbali kujitokeza kudhamini michuano hiyo ili kuwa na michuano bora itakayolenga kuendeleza mchezo huo nchini.
    Fainali za michuano zilifanyika katika Uwanja wa Uhuru, zamani Taifa mjini Dar es Salaam na mgeni rasmi alikuwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambaye naye alifurahia mafanikio ya ligi hiyo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KONDIC AMPOKEA KWA SHANGWE OWINO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top