KOCHA wa timu ya Taifa, Taifa Stars Mbrazil Marcio Maximo ametaja kikosi kitakachomenyana na klabu ya Vancouver ya Marekani, Machi 14, mwaka huu akiwaita chipukizi John Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC, David Naftari wa Simba na George Minja wa JKT Ruvu.
Wengine aliowaita ni 'Tz One' Shaaban Dihile, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Eddy Bushiri kipa wa kikosi cha Zanzibar Heroes na JKU ambaye ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Maximo kwa upande wa makipa. Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam FC), Salum Sued (Mtibwa), Kelvin Yondani, Juma Jabu, David Naftari (Simba), George Minja(JKT Ruvu) na Stephano Mwasika kutoka Moro United. Viungo ni Henry Joseph, Jabir Aziz (Simba), Shaaban Nditi(Mtibwa), Nizar Khalfan (Moro United) na Mwinyi Kazimoto (JKT Ruvu).
Washambuliaji ni Mussa Hassan ‘Mgosi’ (Simba), Zahoro Pazi na Uhuru Selemani (Mtibwa) na Bocco. Kikosi hicho pia wamejumuishwa wachezaji watano kutoka kikosi cha taifa cha vijana chini miaka 20 kwa ajili ya kuwapatia uzoefu na kuwajenga ili waweze kupandisha kuchezea timu hiyo hapo baadaye ambao ni ni Razak Khalfan, Khalid Haji, Furaha Yahaya, Haji Ally Nuhu na Ahmed Hassan.
katika hatua nyingine, Maximo amesema amefunga mjadala wa sakata la wachezaji nyota wa timu hiyo, Haruna Moshi, Athumani Iddi na Amir Maftah, lililoibuka nchini Ivory Coast katika michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) ambako Taifa Stars ilitolewa Raundi ya Kwanza.
Akizungumza leo wakati wa kutaja kikosi cha muda cha Stars, Maximo suala la wachezaji hao waandamizi kwenye kikosi hicho cha Stars kuonekana kususa timu hiyo na kujitenga na wenzao limekuzwa, lakini chanzo cha nyota hao kutofuata programu ya mazoezi na kushindwa kujituma na kuonyesha uzalendo wao kwa taifa, lilianza kabla hawajaenda Ivory Coast. “Suala la Haruna, Iddi na Maftah ni rahisi na jepesi ila limeonekana kukuzwa mno lakini ninachosema ni kuwa wachezaji hao walishindwa kufuata programu ya mazoezi tangu tukiwa Dar es Salaam na hata tulipofika Ivory Coast hali ilikuwa hivyo,” alifafanua Maximo. Maximo alisema hivi sasa soka la Tanzania halina nafasi wala muda wa kupoteza katika mambo yasiyo na msingi, na kusisitiza kinachotakiwa hivi sasa ni wachezaji kufanya mambo hayo kama wachezaji wenye taaluma na kuwa mfano kwa wachezaji chipukizi. Hivi sasa mtazamo wetu ni kuwa na vijana chipukizi wengi zaidi kwenye kikosi cha timu ya taifa ambao tuna hakika watakuwa na malengo ya juu kwa kusaka maendeleo zaidi kisoka ambao watakuwa wakijituma na kufuata programu, ikiwa ni pamoja na kuonyesha uzalendo kwa taifa lao. “Tunataka kuwa na wachezaji wazoefu wa kulipwa ambao watakuwa mfano ndani na nje ya uwanja kwa chipukizi ambao watakuwa kwenye kikosi ili wajifunze kutoka kwao,” aliongeza Maximo. Akizungumzia hali ya kikosi chake wakati wa michuano ya CHAN, Maximo alisema kimedhihirisha kuwa kina nidhamu na kilikwenda kushindana na si kushiriki, tofauti na ilivyokuwa ikifikiriwa hapo awali. Aidha, Maximo amewapongeza wachezaji wa kikosi hicho waliocheza kwa kujituma na kuonyesha uzalendo kwa taifa lao kwa kulitetea kwa uwezo wao wote. Pamoja na timu kuonyesha uwezo kwenye CHAN, Maximo alisema timu hiyo inahitaji kuboreshwa zaidi na kituo cha mazoezi kuimarisha, ikiwa ni pamoja na wachezaji kupelekewa gym kwa ajili ya kujenga miili na kuongeza nguvu, jambo linalotakiwa kwenda sambamba na lishe bora. Wachezaji Moshi ‘Boban’ na Iddi ‘Chuji’ waliingia kwenye mgogoro wa chini chini na kocha Maximo wakati Stars ilipokuwa ikikabiliwa na fainali hizo. Hata hivyo, katika mechi ya kwanza ya Stars dhidi ya Senegal, Maximo alilazimika kumtoa Boban aliyecheza kwa dakika 41 na nafasi yake kuchukuliwa na Musa Hassan ‘Mgosi’ wakati Chuji hakucheza mechi yoyote, kwa madai kuwa mchezaji huyo alikuwa akisumbuliwa na nyama za paja. Sakata hilo lilizidi kuchukua sura mpya na baada ya timu kuwasili ikitokea Ivory Coast, pale wachezaji hao walipogeuka sinema kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa kuwakimbia wanahabari na kutoka mlango tofauti na wenzao na ku
0 comments:
Post a Comment