// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAXIMO: MBELE KWA MBELE TAIFA STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAXIMO: MBELE KWA MBELE TAIFA STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 02, 2009

    MAXIMO: MBELE KWA MBELE TAIFA STARS


    Wachezaji wa Stars wakiogelea kabla ya mechi yao na Ivory Coast, ambayo walishinda 1-0 kwa bao pekee la Mrisho Ngassa.

    na abdul mohammed, bouake
    KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Marcio Maximo amesema kutolewa kwa timu yake katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN) kwa wachezaji wa ligi za ndani si mwisho wa safari. Badala yake Maximo alisema kwamba kilichotokea ni matokeo ya soka na kwamba anaangalia mbele na kuwataka watu wote kwenye timu hiyo kuwa na mtazamo wa aina hiyo. Maximo aliongeza kwamba kutolewa kwa Stars ni somo kubwa kwa wachezaji, Watanzania na kwake mwenyewe. Stars ilitolewa katika CHAN baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Zambia na hivyo kuishia katika hatua ya makundi ikiwa na pointi nne wakati Senegal na Zambia zimeingia Nusu Fainali. Maximo alisema Stars haijawahi kushiriki katika mashindano magumu kama hayo na kumudu kucheza mechi tatu katika kiwango cha kuridhisha katika muda wa siku sita huku wakionyesha ushindani wa hali ya juu. "Hili nalo ni jambo la kuangalia, hatujawahi kucheza mechi ngumu mfululizo namna hiina wacheaji kuonyesha moyo wa kushindana," alisema. Stars ilicheza mechi yake ya kwanza Februari 22 dhidi ya Senegal na kufungwa bao 1-0na kucheza mechi ya pili dhidi ya Ivory Coast Februari 25 na kuibuka na ushindi wabao 1-0 na mechi yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Zambia Februari 28 na kutoka sareya bao 1-1. Maximo alisema tangu mwanzo wa mashindano timu yake ilionyesha moyo wa ushindani, wachezaji walicheza kwa kujituma jambo ambalo anajivunia na hata makocha wenzake wamekiri hilo. Maximo pia alisifu nidhamu ya wachezaji wake na namna ambavyo walionyesha maadili ya soka la kulipwa licha ya matatizo madogo madogo ya hapa na pale ambayo hata hivyo hakuyafafanua. Alisema soka la Tanzania limepiga hatua kubwa na kwamba watu wengi wamekuwa wakiizungumzia Tanzania hususan baada ya kufuzu na hatimaye kushiriki fainali za CHAN.


    KWA NINI TANZANIA IMETOLEWA CHAN...

    na abdul mohammed, yamoussoukro, ivory coast
    KUKOSEKANA kwa umakini katika dakika za mwisho ndilo jambo kubwa lililosababisha kutolewa mapema kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji
    wa ndani (CHAN).
    Akizungumza juzi usiku katika hoteli ya President katika mji mdogo wa Yamoussoukro,
    kocha mkuu wa Stars, Marcio Maximo alisema umakini ulikosekana katika dakika
    za mwisho na hivyo kusababisha timu hiyo ifungwe bao katika dakika za nyongeza.
    Stars juzi ilifungwa na Zambia bao katika dakika tano za nyongeza (94) baada ya
    kupata bao la kuongoza dakika ya 87 lililofungwa kwa penalti na Shedrack Nsajigwa.
    Maximo alisema kwamba kabla ya mechi aliwaambia wachezaji wake kuhusu kuwa makini hadi mwisho wa mchezo na hususan katika mipira iliyokufa ambayo inaweza kubadili matokeo.
    "Baada ya kupata bao tuliona kama mpira umekwisha na kujiona sisi ndio washindi na
    hivyo kuchukulia mambo katika hali ya kawaida lakini mechi ilikuwa haijaisha," alisema Maximo.
    Awali, mara tu baada ya mechi Maximo aligusia suala hilo kwa kusema kwamba katika soka hata sekunde chache tu zinatosha kubadili matokeo.
    Maximo pia alisema wapinzani wao, Zambia ni kati ya timu ngumu na hatoshangaa kama itafika fainali na hata kubeba kombe.
    Alisema kwamba katika timu ya Zambia kuna wachezaji sita ambao walifanya majaribio na wengine kucheza soka Afrika Kusini kabla ya kurudi Zambia na wengine wawili walifanya majaribio Ulaya.
    Aliongeza kuwa kiujumla michuano ilikuwa migumu na ndio maana katika kila mechi alijikuta akibadili wachezaji mara tatu.
    Stars ilizianza fainali za CHAN katika Kundi A kwa kufungwa bao 1-0 kabla ya kuwalaza wenyeji Ivory Coast kwa bao 1-0 na katika mechi yake ya mwisho na Zambia iliambulia sare ya bao 1-1 na hivyo kuziaga fainali hizo.
    Katika Kundi A timu zilizosonga mbele ni Senegal na Zambia ambazo zinasubiri washindi wawili wa Kundi B kwa ajili ya kuumana katika hatua ya Nusu Fainali.


    ...ALIYOSEMA NSAJIGWA BAADA YA KUTOLEWA


    BEKI na nahodha wa Stars, Shadrack Nsajigwa amesema kwamba kilichoikuta Stars katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) ndio mambo ya soka. Stars juzi iliziaga fainali za CHAN baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Zambia katika mechi ambayo kila shabiki aliamini kwamba Stars ingeshinda na kusonga mbele. Nsajigwa ndiye aliyeifungia Stars bao katika dakika ya 87 kwa mkwaju wa penalti lakini Zambia ilisawazisha kupitia kwa Dennis Banda kwa shuti akiunganisha konailiyochongwa kwenye lango la Stars katika dakika za nyongeza. Beki huyo ambaye pia anaichezea timu ya Yanga alisema mechi hiyo ilikua ngumu na kwamba walijitahidi kadri ya uwezo wao kupambana kwa kukabiliana na kasi ya Zambia, lakini mambo hayakuwa mazuri kwa upande wao. "Nawatakia kila la kheri Zambia na naamini watafika mbali, kilichotukuta sisi ni mambo ya soka,' alisema. Nsajigwa pia alisema tatizo la kutokuwa makini nalo lilichangia Stars kutolewa kwani awali walidhani wameshashinda mechi kumbe mambo yalikuwa bado. Stars iliyokua Kundi A matokeo ya sare yameifanya iziage fainali hizo pamoja na wenyeji Ivory Coast huku ikiziacha timu za Zambia na Senegal zikisonga mbele.


    CAF YAWAPIMA MABEKI STARS


    WACHEZAJI wa Stars, Salum Sued na Kelvin Yondan juzi baada ya mechi ya Stars na Zambia, walifanyiwa vipimo ili kujua kama wanatumia dawa haramu michezoni au la. Vipimo hivyo ni sehemu ya utaratibu ulioandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF)kwa lengo la kukabiliana na tatizo la utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu katika soka. Mbali na vipimo hivyo kuhusishwa na dawa za kuongeza nguvu lakini pia vinatumika kubaini iwapo wachezaji hao wanatumia aina nyingine yoyote ya ulevi unaopigwa vita michezoni. Hapo kabla wachezaji waliofanyiwa vipimo vya aina hiyo ni kipa Shaaban Dihile na kiungo Nizar Khalfan waliopimwa baada ya mechi ya Stars na Ivory Coast, mechi ambayo ilimalizika kwa Stars kushinda kwa bao 1-0. Wachezaji wa kwanza wa Stars kufanyiwa vipimo hivyo ni Mrisho Ngassa na Mwinyi Kazimoto ambao walipimwa baada ya mechi na Senegal, mechi ambayo Stars ililala kwa bao 1-0. Akizungumzia vipimo hivyo, Ofisa habari wa CAF, Kabulo Mwana Kabulo ambaye anatokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alisema utaratibu huo ni wa kawaida na utaendelea kufanywa hadi mwisho wa michuano ya CHAN. Hata hivyo Kabulo hakuwa tayari kutaja matokeo ya wachezaji wa kwanza kupimwa kwa upande wa Stars akidai kwamba majibu hayo yatapatikana baadaye. Michuano ya CHAN ambayo ndiyo inafanyika kwa mara ya kwanza ikishirikisha wachezajiwa ligi za ndani inatarajia kufikia kilele chake Machi 8 mwaka huu kwa mechi yafainali ambayo itachezwa katika jiji la Abidjan.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAXIMO: MBELE KWA MBELE TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top