// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MANJI: BILIONEA ANAYEJITOLEA KWA HALI NA MALI YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MANJI: BILIONEA ANAYEJITOLEA KWA HALI NA MALI YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 01, 2009

    MANJI: BILIONEA ANAYEJITOLEA KWA HALI NA MALI YANGA


    WAMEWAHI kutokea wafadhili wengi katika soka ya Tanzania, kuanzia ngazi ya klabu hadi timu za taifa, lakini tathmini inaonyesha Yussuf Mehboob Manji (pichani kulia) ameweka rekodi ya kipekee katika klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.
    Manji ameingia kwenye orodha ya wafadhili wa kukumbukwa Tanzania ambayo inawajumuisha akina Shiraz Sharif, Ahmed Bora, Shafi Bora, Mohamed Virani, Azim Dewji, Abbas Gulamali, Murtaza Dewji, Mohamed Dewji, Naushad Mohamed, Abdulsasattar na Reginald Mengi.
    Lakini mujibu wa historia, Manji anaonekana kufanya mambo makubwa zaidi ya wengine wote, waliotangulia katika ufadhili wa soka ya Tanzania.
    Shiraz Sharif alikuwa mfadhili wa Yanga miaka ya 1960 hadi 1976 alipohamia Pan African, Ahmed Bora alikuwa mfadhili wa Majimaji ya Songea, Shaffi Bora alikuwa Mfadhili wa Simba, Mohamed Virani alikuwa mfadhili wa Yanga aliyejitolea kwa hali na mali enzi za uhai wake kuanzia ujana wake hadi uzee wake.
    Azim Dewji alikuwa mfadhili wa klabu ya Simba, Abbas Gulamali ambaye pia hivi nsasa ni marehemu alikuwa mfadhili wa Yanga, Murtaza Dewji alikuwa mfadhili wa Yanga, Mohamed Dewji alikuwa mfadhili wa Simba ambaye naye alifanya makubwa kwenye klabu hiyo, Naushad Mohamed alikuwa mfadhili wa Malindi, Abdulsasattar alikuwa mfadhili wa Mlandege ya Zanzibar na Reginald Mengi alikuwa akiisaidia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
    Kwa kipindi cha miaka mitatu ya kuifadhili klabu hiyo, Manji ameifanya Yanga kuwa klabu yenye mwonekano mzuri zaidi ndani na nje, ingawa uongozi bora bado ni tatizo kwenye klabu hiyo.
    Manji aliyeanza kuifadhili Yanga Juni mwaka 2006, mbali na kuiwezesha klabu hiyo kusajili kikosi imara kinachotamba kwenye soka ya Tanzania, pia ameitengenezea misingi mizuri klabu hiyo, ambayo kama itatumika vizuri kwa siku zijazo inaweza kujiendesha yenyewe.
    Misingi hiyo ni kukarabati jengo lake kuu liliopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, ambalo likikamilika litakuwa la kisasa kabisa.
    Jengo hilo litakuwa na vyumba vinavyojitegemea (self contained), vyenye viyoyozi (air conditions) ndani na thamani (feniture) za kisasa, hivyo kufanya hosteli nzuri ambayo wakati mwingine Yanga inaweza kuitumikia kama kitega uchumi.
    Aidha, kwenye jengo hilo kutakuwa eneo la mazoezi la mazoezi ya viungo (gym), bwawa la kuogelea, eneo la kupumzikia, sehemu ya chakula na eneo la wachezaji au wageni kupumzika wakiendelea na michezo midogo midogo ya kujiburudisha kama pooltable.
    Manji pia anaitengenezea klabu hiyo Uwanja, ambao utakuwa na nyasi za bandia na kusimamisha uzio utakaotengeneza mandhari nzuri.
    Yote hayo yanakuja baada ya juhudi za awali kabisa za Manji kuzima mgogoro mkubwa uliokuwa ukiisumbua klabu hiyo tangu miaka ya 1990, ambao wengi waliojaribu kujitosa kuusuluhisha ikiwemo viongozi wa serikali na mfanyabishara maarufu na mpenzi wa klabu hiyo, Reginald Mengi walishindwa.
    Lakini kwa ujasiri wake, Yusuf alijitosa na kupambana na fikra za zilizokuwa zikipingana wakati huo hadi kuziweka pamoja, hatimaye ule uliokuwa unaitwa mgogoro wa Yanga Kampuni na Yanga Asili, ulizikwa na ikarejeshwa Yanga moja tu, ile inayobeba kaulimbiu, daima mbele, nyuma mwiko.
    Kinara wa lililokuwa kundi la Yanga Asili, Yussuf Mzimba na yule wa lililokuwa kundi la Yanga Kampuni, Francis Kifukwe walipeana mikono na kuunganisha nguvu zao, kuelekea katika kuisimamisha vizuri.
    Hatimaye Mei mwaka juzi ulifanyika uchaguzi ulioshirikisha pande zote mbili, zilizokuwa zikipingana na ikapatikana safu mpya ya viongozi wanaoungwa mkono wana Yanga wote, chini ya Mwenyekiti Imani Madega.
    Wakati wana Yanga wakiwa wanaongea lugha moja, Manji aliendelea jitihada zake za kuifanya klabu hiyo iwe ya kipekee, akitumia fedha nyingi kuwasaidia kwa mambo mbalimbali hata sasa imefikia mfanyabishara huyo ni kipenzi cha wana Yanga.
    Mapenzi wa Yanga kwa Manji yalionekana wazi kipindi kile alichokuwa akisumbuliwa na maradhi ya malaria hadi kuhamishwa kutoka hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam hadi Aga Khan ya Nairobi.
    Ni kipindi hicho Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega alipolazimika kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari mara kwa mara juu ya hali ya kiafya ya mfadhili wao huyo, ili kutuiliza nafsi za wana Yanga.
    Manji alianza kusumbuliwa na Malaria siku chac he tu baada ya Yanga kuifunga Simba 1-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Oktoba 26 mwaka jana, siku ambayo bao pekee la Ben Mwalala dakika ya16 liliipa ushindi timu aipendayo.
    Alipopona, Manji ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Quality Group Limited aliibuka na kusema kwamba alikuwa anasumbuliwa na maralia ya kawaida na hakuwa na hali mbaya kiasi cha kuibuka habari za kuzushiwa kifo.
    Lakini Manji alisema kwamba, kitendo cha wana Yanga kuwa na huzuni kilitokana na klabu kuwa tegemezi, inamtegemea Manji na kusahau kuwa yeye ni mwanadamu wa kawaida ambaye ana mwisho wake.
    “Lazima nitakufa siku moja, Yanga inapaswa kujitegemea, sasa si timu ndogo tena, na hiyo ndio imekuwa sehemu kubwa ya malengo yangu. Nimetaka kuisaidia Yanga, lakini siwezi kuisaidia milele,”alisema Manji na kunukuliwa na gazeti la Mwanaspoti.
    “Inatakiwa kuwa timu inayojitegemea hata kama kuna wengine wanaisaidia. Unajua Yanga ni timu tajiri kuliko nyingine hapa Tanzania, kama utapiga hesabu, mimi nakutolea mfano mmoja.
    Pale uwanjani katika mechi kati ya Simba na Yanga takribani watu 40,000 uwanjani walikuwa Yanga. Sasa kama hao wakilipa ada ya uanachama, yaani Sh 1,000 kwa mwezi kila mmoja inakuwa Sh 12,000 kwa mwaka halafu unazidisha mara 40,000 inakuwa ni Sh milioni 480.
    Angalia hapo, hao ni watu tu walioingia uwanjani, idadi ya chini kabisa ya mashabiki wa Yanga tufanye kwa Tanzania nzima ni watu milioni 10, wote wakilipa ada ya mwaka mzima itakuwa Sh bilioni 120 kwa mwaka.
    Sasa jiulize kama timu ina uwezo wa kuingiza fedha kama hizo kwa mwaka, wanataka nini zaidi? Utaona kuna kitu kimoja hapa, kwamba kama ada ya mwezi ni Sh 1,000 tu maana yake kila mtu anaweza kulipa na kama ana mapenzi ya kweli na Yanga anaweza kutoa ada na kuwa mmiliki wa timu yake.
    manji alisema yeye ni mpenzi wa Yanga na aliyeanza kuishabikia klabu hiyo, tangu akiwa mdogo.
    “Niliendelea kufanya hivyo nikiwa chuo nchini Uswisi na baadaye Marekani kwa kuwa baba yangu mzazi, Mahboob Manji alikuwa ni shabiki mkubwa wa Yanga,”alisema.
    Manji ambaye pia ameajiri makocha watatu kutoka Serbia, Dusan Kondic, Spaso Sokolovski na Civojnov Serdan, pia amesajili kipa kutoia Serbia Obren Curkovic ambaye anasifika kutokana na udakaji wake mzuri.
    Manji ameirejesha juu tena Yanga dhidi ya watani wao wa jadi, Simba ambao sasa wasuasua kwenye soika ya Tanzania.
    Aliwakata maini kabisa Simba baada ya kutoa fungu lililotumika kumsajili kipa hodari na kipenzi cha wana Msimbazi, Juma Kaseja.
    Hata hivyo, tangu siku ya kwanza wanachaguliwa viongozi wa sasa, chini ya Madega, Manji aliwaambia kabisa dhamira yake ni kuifanya Yanga ijitegemee, kwani anaamini inaweza.
    “Najivunia ilipofikia Yanga ingawa sioni kama kazi imefika mwisho bila ya kujitegemea. Msimu mmoja tumeweka rekodi nyingi sana, kuhusu makocha, wachezaji na hata kuchukua wachezaji watatu kutoka Simba kwa wakati mmoja,”alisema Manji ambaye ni baba wa watoto wawili, Mahboob-Mahboob na Mahboob-Ally.
    Yusuf Mehboob Manji, aliyesomea uongozi wa biashara katika vyuo vikuu vya Uswisi na Marekani amekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya Quality Group tangu mwaka 1995.
    Kwa hakika wamejitokeza wengi kufadhili mchezo huu nchini Tanzania, lakini Manji amefanya makubwa zaidi. Hiyo ni bahati ya mtende iliyowaangukia wana Yanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANJI: BILIONEA ANAYEJITOLEA KWA HALI NA MALI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top