// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KILIMANJARO YAMWAGA VIFAA YANGA, TIMU KAMBINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KILIMANJARO YAMWAGA VIFAA YANGA, TIMU KAMBINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 05, 2009

    KILIMANJARO YAMWAGA VIFAA YANGA, TIMU KAMBINI


    Hapa Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Oscar Shelukindo akimkabidhi vifaa Katibu Mkuu wa Yanga, Lucas Kisasa.

    YANGA imepanga kambini rasmi leo mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Al Ahly ya Misri.
    Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Lucas Kisasa, alisema hayo leo baada ya kupokea jezi kutoka kwa wadhamini wa klabu hiyo kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro kwa ajili ya mechi dhidi ya Al Ahly. Kisasa alisema baada ya wachezaji wao walioko Taifa Stars kurejea nchini jana wakitokea Ivory Coast, kambi rasmi inaanza kujiandaa kuwakabili mabingwa watetezi hao kwa ajili ya mchezo huo ambao utafanyika Cairo, Misri Machi 15. Pia Kisasa alisema kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kuondoka nchini Jumanne kwenda Misri kwa ajili ya mchezo huo na kusema vifaa walivyopewa na TBL ni changamoto yao ya kufanya vizuri katika mechi zao mbili, ile ya Cairo pamoja na itakayofanyika Dar es Salaam wiki mbili baada ya mchezo wa Cairo. “Pamoja na kutambua tunakwenda kucheza na timu kali na ngumu barani Afrika, matarajio yetu ni kuendeleza wimbi la ushindi tuliloanzisha katika raundi ya awali,” alisema Kisasa. Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Oscar Shelukindo alisema wao kama wadhamini ni wajibu wao kutoa motisha na lengo lao ni kuhakikisha Yanga inafanya vema kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa. Kwa mujibu wa Shelukindo, vifaa vilivyotolewa kwa timu ya Yanga vina thamani ya Sh milioni 6.3, jezi hizo seti mbili zilitolewa kwa ajili ya mechi dhidi ya Al Ahly. Jezi zitakazotumika kwenye mchezo wa ugenini zina rangi ya kijani tupu na ina michirizi ya njano kutoka mabegani na ubavuni kwenda chini na zile zitakazotumika kwenye mechi itakayofanyika Dar es Salaam ni za rangi za njano tu na michirizi midogo ya kijani mabegani na ubavuni. Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Yanga, Kisasa ametoa ufafanuzi kuhusu suala la mshambuliaji wao wa kimataifa kutoka Kenya, Boniface Ambani ambaye amekwenda China, kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa. Kisasa alisema mchezaji huyo aliyeondoka mwishoni mwa wiki atarejea Dar es Salaam Jumatatu ijayo siku moja kabla ya safari ya Misri ambaye naye yumo kwenye orodha ya kikosi kitakachokwenda kuikabili Al Ahly. Kisasa amekana taarifa kuwa mchezaji huyo mara baada kuondolewa kwenye Hoteli ya Lamada Dar es Salaam walikokuwa wakiishi na wenzake kutoka Kenya na kipa Mserbia Curkovic Obrien kuwa Yanga wamevunja baadhi ya makubaliano ya mkataba wake, ndio maana ameamua kuondoka. Yanga iliwatoa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa kwenye raundi ya awali timu ya Etoile d’or Minorsty ya Comoro kwa jumla ya mabao 14-1.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KILIMANJARO YAMWAGA VIFAA YANGA, TIMU KAMBINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top