“NIMECHEZA michuano mingi ya kitaifana kimataifa tangu nikiwa nacheza ngumi za ridhaa na baadaye kujiunga na ngumi za kulipwa, lakini katika hiyo yote sitasahau mchezo ambao nilipambana na bondia wa Korea Ungel Kim Yung.
Mchezo huo ulikuwa katika mfululizo wa michuano ya Olimpiki iliyofanyika mjini Munich, Ujerumani mwaka 1972 na mimi nilikuwa mmoja kati ya mabondia waliounda kikosi cha timu ya Taifa Tanzania.
“Kwa kweli miaka yote timu za Tanzania huwa zinalalamikiwa na maandalizi, lakini mwaka huo tulijiandaa vizuri mno katika muda wa kutosha kwenye kambi yetu iliyokuwa chuo kikuu cha Dar es Salaam.
“Tulikuwa chini ya kocha mwenye utaalamu mkubwa juu ya mchezo wa ndondi, Calvin Cohwen kutoka Marekani ambaye alituandaa kwa miezi minne kambini huko mlimani, chuo kikuu. Alitupa mazoezi ambayo yalitujenga vizuri na kila mmoja wetu alikiri yeye ni mwalimu wa Kimataifa.
“Siku tunaondoka baada ya kukabidhiwa bendera ya Taifa nilikuwa nikiwaza sana juu ya bondia ambaye nitakumbana naye huko kwenye michuano ya Olimpiki ambayo ni miongoni mwa michezo mikubwa inayoheshimika sana duniani.
"Mabondia wenzangu wa timu ya Taifa walikuwa wakiniambia kuwa kutokana na uzito wangu wa chini, basi kama ni bondia wa Korea, Mexico au Japan, basi nitakumbana na bondia wa Cuba ambao wote wanasifika kwa mchezo mzuri.
“Lakini kwa kuwa maji nimeshayavulia nguo, sikuwa na sababu yo yote ya kukwepa, hivyo nikapiga moyo konde na kusema yeyote atakayetokea mbele yangu lazima nimmalize. Basi hiyo ilinipa faraja na kupata kausingizi kwenye ndege ambako kilinizindua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Munich
"Tulipoteremka tu na kwenda kwenye kambi yetu, siku iliyofuata nilikwenda kupima uzito kwa ajili ya kupangiwa mpinzani tutakayekumbana nae kwenye fungua dimba ya michuano hiyo.
“Looh, kama ambavyo wenzangu walikuwa wakisema kwamba kama si Mkorea basi ningekumbana na Mmexico au Mjapani na Mcuba, basi ndivyo ilivyokuwa, kwani ratiba iliyotoka bondia wa Light Fly Tanzania alipangwa kupambana na Mkorea.
“Huyo alikuwa ni Ungel Kim Yung, mbabe mfupi aliyesheheni misuli ya nguvu. Kocha wangu Calvin aliniita na kuniambia kuwa kutokana na jinsi nilivyojiandaa ana imani kuwa nitashinda hasa endapo nitayazingatia mafunzo yake ulingoni.
“Alinionya kutokuwa mwoga ulingoni kwa kuwa ile ilikuwa mara yangu ya kwanza kupanda ulingoni kwenye mashindano makubwa kama yale. Kwa kuwa nilikuwa na asili ya kutomuogopa mtu yeyote yule tangu utotoni ilikuwa rahisi kuyazingatia maoni yake.
“Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, kwani siku ya pambano nilijawa na ujasiri mkubwa mno na hamu yangu ilikuwa ni kuona Mkorea anakaa chini kwenye raundi ya kwanza ya pambano hilo la ufunguzi.
“Kama ilivyo kawaida kwamba kwenye mapambano lazima mabondia wa uzito wa chini ndio wanaoanza, basi pambano letu lilikuwa la kwanza la kufungua pazia la mashindano.
Pembeni yangu alikuwepo kocha Calvin, raundi ya kwanza kwa mimi kuonyesha kumzidi uwezo mkorea kwa kumpiga ngumi mfululizo, hali iliyowafanya wajerumani washangilie kwa juhudi kubwa.
“Hiyo ilimpa moyo hata kocha wangu wakati nikimuweka kwenye kona Mkorea akinipigia makelele ya kunitaka niongeze kazi ili Mkorea akae chini nami nipate ushindi wa Knockout (KO).
Hata mabondia wenzangu nao walikuwa wakinipigia kelele mno, Bakari maliza, maliza kaisha huyo, maliza hapo hapo bado ngumi moja aende chini.
“Lakini looh, mambo hayakuwwa kama wenzangu walivyokuwa wakiniombea, kwani kengele ya kumaliza raundi ya kwanza ililia wakati Mkorea akiwa bado yuko sawa sawa tena imara mno.
“Dhana yangu, wenzangu pamoja na kocha kuniambia raundi ya pili nitamaliza kazi niliyoshindwa kuimaliza raundi ya kwanza kwa kumkalisha chini Mkorea. Kumbe hiyo ilikuwa ni kinyume kabisa, kwani hapo Mkorea alikuja akiwa na nguvu mpya katika raundi ya pili.
“Bila shaka ni baada ya kuusoma mchezo wangu na kunielewa, kwani alianza kunikwepa kila nikimvamia kisha kinitwnga ngumi za ujanja mno na kuhama sehemu nyingine kisha kuja tena kunitwanga na kuhama hadi nikazidiwa mno.
“Ilifika wakati katika raundi hiyo ya pili nikalewa mno na kila mmoja akajua wakati wowote ningeanguka, kocha akaanza kunipigia kelele ulingoni na kuhoji kulikoni mambo yamegeuka gafla.
“Lakini wapi hiyo haikuwa dawa, Mkorea aliendelea tu kunitwanga jinsi anavyotaka, nikienda huku ananipa (ngumi), nikirudi huku ananipa hadi nikalewa kabisa, sasa kilichobaki nikajifanya nunda asiyesikia kitu ulingoni ili niweze kumaliza pambano.
“Kocha akawa ananipa mbinu za kuepuka mkongoto wa Mkorea huku pambano likiendelea lakini wapi, kila nilivyojaribu kufanya anavyotaka mambo hayageuki, napigwa yaani kwa kweli alinizidi uwezo ile mbaya.
“Raundi ilipokwisha niliwekwa chini huku nikipepewa ulingoni kisha kocha kuniambia kuwa pambano likianza nimvamie yeye nisingoje anianze halafu nijitahidi mno kuhakikisha anakuwa katika himaya yangu mimi nisiingie kwake
“Mbinu hizo ziliniingia vizuri kichwani na kuanza katika raundi ya tatu na ya mwisho ya pambano lile. Lakini bado mambo hayakuwa shwari, kwani mikongoto niliendelea kuipokea kama kawaida.
“Raundi ilipoanza nilimvamia kama alivyoagiza kocha, lakini alinipisha na kunipa ngumi mbili tatu kisha kuniingiza kwenye himaya yake na kunitwanga hadi nikalewa, sasa hapo yale yote aliyonipa Mkorea yalirejea kwao na mimi kuwa gunia la mazoezi la Kim Yung.
“Kilichonisaidia kwa kiasi kikubwa ni ununda wangu ulingoni kwa kuvumilia kipigo cha Mkorea yule. Lengo likawa kukwepa kupata kipigo cha KO, nilikuwa nikivumilia kadiri alivyonipiga hadi nikamaliza pambano.
“Hata hivyo, watu wengi walinipongeza baada ya pambano kwani nilipambana na bondia aliyekuwa wa kiwango cha juu kuliko changu. Yeye alikuwa na uzoefu ya michuano ya kimataifa wakati mimi ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza napigana kwenye mashaindano ya kimataifa.
“Kudhihirisha kama Ungel Kim Yung alikuwa kiboko ndiye aliyekuja kutwaa Medali ya Dhahabu ya michuano ile katika uzito ule. Lakini cha kujivunia katika michuano iliyofuata sikutolewa tena raundi ya kwanza, Ilikuwa nakwenda hadi kwenye Medali aidha ya Shaba au Fedha kama si Dhahabu.
“Kwa kweli hadi siku inapigwa parapanda sitaweza kuusahau mchezo huo. Mbinu zote za kocha Mmarekani zilishindwa kufua dafu kwa Mkorea Ungel Kim Yung. “Hiyo ndiyo mechi ninayoikumbuka kuliko zote nilizocheza enzi zangu”.
WASIFU WAKE:
Jina:Bakari Selemani Tanda ‘Match Maker’
Umri: Miaka 52
Mchezo: Ngumi za Ridhaa/Kulipwa
Uzito: Light Fly
Timu alizowahi kuchezea: Magomeni BC na timu ya Taifa.
Kazi: Dereva, kocha na refa Ndondi

0 comments:
Post a Comment