OBRIEN Curkovic, kipa Mserbia wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, amehamishiwa katika hoteli ya Travertine, Magomeni mjini Dar es Salaam baada ya kufukuzwa katika hoteli ya Lamada, Ilala jijini.
Habari kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba kipa hiyo anaishi kwenye hoteli hiyo pamoja ns mshambuliaji Mkenya, Mike Barasa.
“Wale wengine wanne ndio waliopangia nyumba Sinza, lakini hawa nao wamehamnishwa pale baada ya uongozi wa Yanga kutofautiana na uongozi wa Lamada,”kilisema chanzo chetu kutoka Yanga.
Wachezaji waliopangiwa nyumba Sinza ni Boniphace Ambani, Ben Mwalala, Maurice Sunguti na George Owino.
Jumatano wiki hii, wachezaji hao walifukuzwa Lamada walipokuwa wakiishi, ingawa baadaye Mwenyekiti wa klabu hiyo, Imani Madega aliibuka na kusema kwamba wamesitisha kulipia malazi ya nyota hao hapo, kwa kuwa wamekwishawapangia nyumba siku nyingi Sinza lakini hawataki kuhamia.
“Tulisitisha malipo tulipoona wanagoma kuhama, hatuwezi kubembeleza wachezaji fulani wakati timu ni ya wachezaji wote waliosajiliwa,” alisema Madega.

0 comments:
Post a Comment