Hapa Ambani yupo na mwanasoka bora wa zamani Afrika, Kalusha Bwalya wa Zambia.
AKIICHEZEA timu ya Greentown FC ya Guangzhou, China, Boniphace Ambani juzi alifunga bao la kwanza, dakika ya pili sekunde ya kwanza, wakati timu hiyo inaibuka na ushindi wa mabao 3-2 kwenye mchezo wa kirafiki.
"Nimecheza mechi yangu ya kwanza leo, kwenye hali ya baridi kali, lakini nimefunga bao dakika ya pili tu, nashukuru nimefunga bao zuri sana, jamaa wamenikubali sana hapa,"alisema jana Ambani alipozungumza na bongostaz kwa simu kutoka China.
Alisema Ijumaa atacheza mechi yake ya pili ya majaribio na baada ya hapo, Jumamosi atapanda ndege kurejea Dar es Salaam kuungana na timu yake kwa ajili ya mechi ya Raundi ya Kwanza, Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Timu hiyo imemuita Ambani, mchezaji wa Yanga kwa majaribio ili ikiridhika naye imsajili. HABARI KAMILI KUHUSU AMBANI SOMA DIMBA JUMAPILI.
0 comments:
Post a Comment