BONIPHACE Ambani, mshambuliaji wa Yanga (pichani) ambaye amekwenda China kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Greentown ya Guangzhou, amefuzu baada ya kucheza soka safi katika mechi ya leo na kufunga tena bao tamu dakika ya nne tu ya mchezo, ingawa timu yake ililala 3-2.
"Tumefungwa 3-2 leo, lakini namshukuru Mungu nimefunga bao la kwanza kwa mara nyingine, kwenye dakika ya nne. Narejea tarehe kumi, sasa imebaki kwa Yanga kumalizana na hii klabu,"alisema Ambani kwa simu kutoka China alipozungumza na bongostaz.
Ambani alisema kwamba wakala wake amemuambia kwamba Greentwon imemkubali kupita kiasi na mara moja inaanza mawasiliano na Yanga juu ya kumnunua. Hii inakuwa mechi ya pili mfululizo ya majaribio, Ambani akiichezea timu hiyo ya Ligi Kuu ya China na kufunga bao, katika mchezo wa kwanza Jumanne, Ambani pia alifunga dakika ya pili wakati timu hiyo ikiibuka na ushindi wa 3-2. Ambani aliondoka nchini Jumapili iliyopita kwenda China, baada ya kuruhusiwa na uongozi wa klabu hiyo kwenda kufanya majaribio. HABARI KAMILI KUHUSU AMBANI NA VITU VYAKE ALIVYOFANYA HUKO, USIKOSE DIMBA JUMAPILI.
0 comments:
Post a Comment