Wema akivutwa mkono na mama yake waende nyumbani, baada ya kutoka mahakamani
Wema akimbembeleza Jumbe aende nyumbani, ili yeye aondoke na mama yake
Hapa ni safari kuelekea nyumbani, Wema akisongeshwa na mama yake

MREMBO wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu jana alizua kizaazaa muda mfupi baada ya kuachiwa kwa dhamana katika kesi inayomkabili ya kuvunja kioo cha gari cha msanii Stephen Kanumba chenye thamani ya Sh milioni moja. Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Kinondoni, Emilius Mchaulu ambapo mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu alisaini dhamana ya Sh 500,000. Wema anatarajiwa kurudi mahakamani hapo Machi 18, mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa. Mamia ya watu walifurika mahakamani hapo kufuatilia kesi hiyo, ambapo wengi walizunguka kumsikiliza wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani. Hata hivyo hali ilikuwa tofauti nje ya mahakama hiyo, ambapo Wema alikataa kupanda gari aina ya Pajero lililokuja na ndugu zake kumchukua, badala yake alionekana akihangaika huku na kule kana kwamba kuna mtu alikuwa akimtafuta. Wema alitumia dakika kadhaa kujibizana na ndugu zake nje ya mahakama hiyo, dakika chache baadaye alishtuka na kumkimbilia kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Jumbe Yusuph na kumkumbatia kisha kumbusu mara kwa mara. Tukio hilo lilionekana kuvuta hisia za watu wengi waliokuwapo mahakamani hapo, baadhi yao walikuwa wakimzomea na wengine wakiwa wanawasogelea. Baadaye kijana huyo ambaye ilidaiwa ni mume wake aliondoka na Wema akiwa amemshika mkono, huku akisindikizwa na wapambe wake mpaka katika kibaraza cha nyumba moja pembeni ya mahakama hiyo. Kufuatia hali hiyo ndugu zake Wema wakiongozwa na mama yake mzazi walimfuata binti yao mpaka eneo hilo na walimchukua kwa nguvu huku mama yake akitishia kumfutia dhamana aliyomwekea. “Nakwambia twende nyumbani haraka, kama sivyo ninakufutia dhamana yako sasa hivi, ili urudishwe rumande haraka,” alisikika mama huyo akisema. Wema alitii amri hiyo na kuondoka na mama yake, ambapo alipandishwa gari hiyo iliyokuja na familia na kupelekwa nyumbani kwa dada yake Sinza, Dar es Salaam. Akizungumza na gazeti hili kuhusiana na tukio hilo, mama yake Wema, alisema ameamua kumchukua Wema kwa kuwa hamtambui Jumbe kama mume wa Wema. Akifafanua mama huyo alisema hawajawahi kusikia kama kuna mtu anaweza kuoa bila ya kutambulishwa katika familia anayoenda kuoa. Alisema wataendelea kumshikilia Wema mpaka ahakikishe kuwa anabadilika tabia tofauti na ilivyo sasa. Mama huyo alisema maneno mengi kwa hasira, akisisitiza hatambui mwanawe kuolewa na kijana huyo.
MEREY APANDISHWA KIZIMBANI
MKURUGENZI Mtendaji wa Dar es Salaam Cement na mfanyabiashara maarufu nchini, Merey Ally Merey (41) na mwenzake, Abdallah Said Abdallah (48), jana walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kuunganishwa katika kesi ya wizi wa fedha katika benki ya Barclays.
Merei, ambaye pia ni mdau mkubwa michezo na Abdallah, waliunganishwa kwenye kesi hiyo pamoja na washitakiwa wengine saba, ambao jana hawakuwapo mahakamani wakidaiwa kula njama na kuiba zaidi ya dola za Marekani milioni moja.
Washitakiwa hao waliunganishwa na watuhumiwa wengine katika mashitaka ya kwanza, ya pili, tisa na 10 ya kula njama, kugushi, huku katika kosa la 11 na 12 ya wizi, yakiwahusu washitakiwa wa nane na tisa, Merey na Abdallah.
Akiwasomea shitaka la kwanza linalowakabili, Mwendesha Mashitaka Mkuu, Charles Kenyela, alidai kuwa Oktoba 19, mwaka jana, washitakiwa hao na washitakiwa wengine saba ambao wako nje kwa dhamana, walikula njama za kuiba dola za Marekani 1,263,000, mali ya Benki ya Barclays.
Mbele ya Hakimu Mkazi Walyalwande Lema, katika shitaka la tisa Merey na Abdallah, Oktoba 27, mwaka jana walidaiwa kughushi ujembe wa kasi wenye namba 000305 kupitia akaunti namba 00180093 uliokuwa akienda Kampuni ya Mafuta ya Oilcom kwa lengo la kuhamisha dola za Marekani 700,769, wakidai ulikuwa halali.
Kenyela alidai kuwa katika shitaka la 10 lililotokea Oktoba 27, mwaka jana jijini Dar es Salaam, washitakiwa hao walighushi ujembe wa kasi kwa lengo la kuiba dola za Marekani 299,974.
Shitaka la 11 na 12 linawahusu washitakiwa wa nane na tisa, Merey na Abdallah, ambako ilidaiwa kuwa Oktoba 30, mwaka jana, kwa nyakati tofauti katika Benki ya Barclays, Tawi la Ohio, waliiba jumla ya dola za Marekani 1,000,943 mali ya benki hiyo.
Washitakiwa hao wanaotetewa na Mawakili wawili, Martin Matunda na Walter Chipeta, walikana kuhusika na mashitaka yote na kudhaminiwa kwa hati ya mali yenye thamani ya Sh milioni 900.
Washitakiwa hao walidhaminiwa kwa masharti yaliyowekwa na Mahakama Novemba 13, mwaka jana, ambayo ni kuwa na wadhamini wawili kila mmoja, waliotakiwa kusaini bondi ya Sh milioni 40, kutoa fedha taslimu Sh milioni 78 na au kuweka mali yenye thamani hiyo, kutotoka nje ya jiji la Dar es Salaam bila kibali cha mahakama na kuwasilisha hati zao za kusafiria mahakamani.
Merey, maarufu katika michezo kwa jina la Balhabou, alikuwa mmiliki wa timu ya Moro United akiichukua kutoka madaraja ya chini ilikokuwa ikifahamika kama Zaragoza na kuipandisha daraja.
Amewahi kuwa mlezi wa Chama cha Waandishi wa Michezo nchini (TASWA).
Washitakiwa hao walidhaminiwa na Ipyana Mwandemba, dereva wa Ubalozi wa Comoro nchini, Said Awadh, anayefanya kazi Ubalozi wa Comoro, Sahau Kambi, ambaye ni mshauri wa Balozi wa Comoro nchini na dereva wa Balozi huyo, Paul Fernandez.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Winford Mwang’onda (34), Shubira Mutungi (24), Neema Saria (24), Upendo Mushi (30), Margaret Longway (31), Emmanuel Mukono (40) na Ramadhani Khamis (36). Kesi hiyo itatajwa April 29, mwaka huu.

0 comments:
Post a Comment