// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAXIMO: WATOTO WALICHEZA TOFAUTI NA MIPANGO YANGU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAXIMO: WATOTO WALICHEZA TOFAUTI NA MIPANGO YANGU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, February 24, 2009

    MAXIMO: WATOTO WALICHEZA TOFAUTI NA MIPANGO YANGU


    na abdul mohammed, abidjan
    KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Marcio Maximo amesema kwamba timu yakeilicheza chini ya kiwango katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrikakwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN)Stars juzi ilifungwa bao 1-0 na Senegal ikiwa ndio mechi yake ya kwanza ya michuanohiyo.Hata hivyo Maximo hakuwa tayari kutaja majina ya wachezaji hao waliovurunda mmoja mmoja akidai kwamba jambo hilo ni sawa na kuwakatisha tamaa."Kama ni kuzungumza na wachezaji jambo hilo nalifanya kwa wakati wangu nikiwa nao, siwezi kutaja majina ya wachezaji lakini hata nyinyi mlikuwa uwanjani mliona," alisema.Mmoja wa wachezaji ambaye juzi alionekana kucheza chini ya kiwango ni Haruna Moshiambaye hata hivyo Maximo alimtoa mapema na nafasi yake kuchukuliwa na Mussa Hassan Mgosi.Mchezaji mwingine ni Geofrey Bonny ambaye aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Abdi Kassim. Awali mara tu baada ya mechi, Maximo alisema kwamba alitegemea matokeo kuwa sare ya bao 1-1 lakini hali ilikuwa tofauti kwani wapinzani wao waliitumia vizuri nafasi moja waliyoipata.Katika hatua nyingine Maximo alisema kwamba kinachohitajika kwa sasa ni kuaminikatika mkakati wa kuandaa kizazi kipya cha wachezaji.Aliwataja wachezaji Jerry Tegete, Mwinyi Kazimoto; Mrisho Ngasa ni sehemu yawachezaji wanaotakiwa kuwa katika mfumo wa kuendelezwa kwani iwapo watapotea mambo yatakuwa mabaya zaidi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAXIMO: WATOTO WALICHEZA TOFAUTI NA MIPANGO YANGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top