KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, taifa Stars, Marcio Maximo kwa pamoja na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), juzi walimuweka chini kiungo tegemeo wa timu hiyo, Haruna Moshi ‘Boban’ na kuzungumzia naye.
Sababu ya Maximo na viongozi hao kuzungumza na Boban ni kutokana kucheza kwake ovyon kwenye mechi ya kwanza ya CHAN, Jumapili dhidi ya Senegal na kusababisha bao pekee lililoizamisha Stars siku hiyo.
“Kwa kweli kocha amekaa naye, amezungumza naye, na sisi tulizungumza naye, tunaamini ameelewa, yeye akiwa mchezaji tegemeo anapaswa kujituma uwanjani,”alisema Katibu Mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela alipozunguzma kwa simu na DIMBA jana asubuhi.
Mwakalebela alisema kwamba kambi ya Stars iko vizuri na anaamini kabisa mchezo wa leo dhidi ya Ivory Coast vijana watashinda kwani wote sasa wanajua mechi hiyo ndio imebeba mustakabli wao.
“Kwa kweli vijana wameahidi kupigana kiume ili washinde leo, wamesema waliiona Ivory Coast ilipocheza na Zambia, safu yao ya ulinzi ni butu, kwa hivyo tuombe Mungu,”alisema Mwakalebela.
Boban alitolewa na Maximo dakika chache kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza, baada tu ya kusababisha bao lililoizamisha Stars siku hiyo. Hata hivyo, katika mchezo wa leo, Maximo atamuanzisha tena kiungio huyo wa Simba, ambaye kama atacheza kwa ari na kujituma atakuwa msaada mkubwa kwenye timu.
Wengine wanaotarajiwan kuanzishwa leo ni viungo Athumani Iddi ‘Chuji’ na Kiggi Makasy ambao wote walikosa mchezo wa kwanza kwa sababu mbalimbali.
Wakati Kiggi alikuwa anatumikia adhabu ya kadi za njano, Chuji alikuwa nje kwa sababu ya maumivu.
0 comments:
Post a Comment