Dar es Salaam, Januari 26, 2009
Zain Group, imetajwa kuwa kampuni bora ya mawasiliano inayoongoza Afrik na Mashariki ya Kati mwaka 2008 na jarida la biashara linaloongoza la Comms MEA.
Tuzo hizo zilitangazwa Grand Hyatt Dubai Desemba 15, ambapo kampuni ya Zain’s Bahrain ilitangazwa kuwa kampuni bora ya mawasiliano Mashariki ya Kati.
Zain imeunganisha shughuli zake na mtandao mmoja na kuunganisha masoko na kuleta mabadiliko makubwa kupitia huduma yake ya One-Network, huduma ya kwanza duniani kuunganisha mabara mawili ambayo ni Afrika na Mashariki ya Kati.
"Kinachodhihirisha mafanikio haya ni kwamba miaka saba iliyopita Zain ilikuwa na mtandao katika nchi moja tu ya Kuwait ikiwa na wateja 600,000 tu. Lakini leo hii ni kampuni kubwa ya mawasiliano inayohudumia wateja milioni 56 katika nchi 23," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Khaled Muhtadi (PICHANI JUU KULIA).
Zain ilibadilisha jina lake la biashara katika shughuli zaka barani Arika mwaka jana kutoka Celetel kuwa Zain na inaeendelea kupanua shughuli zake katika masoko mapya, soko la hivi karibuni likiwa la nchini Ghana ambapo iliwaha mitambo yake mwezi uliopita.
Kabla ya Ghana, Zain ililipa dola za Marekani 1.2 billion kununua Iraqna nchini Iraq, mtandao ambao una zaidi ya wateja milini tatu. Biashara ya Zain Saudi Arabia ambayo ilianza mwezi Agosti mwaka jana pia imeanza kutoa gawiwo kwa wenye hisa na wateja wameshavuka milioni moja.
Miradi mingine ya kupanuka kwa shughuli za Zain imefanyika wakati wa misukosuko ya kuichumi duniani, ambapo katika kipindi hico pia Zain iliweza kukusanya mtaji wa dola za Marekani 4.5 bilioni.
Zain ilitumia Dola za Marekani milioni 120 kununua Ghana’s Westel, ambayo ndio kamupini ya hivi karibuni kununuliwa na Zain Barani Afrika. Zain ilizindua huduma hizo pamoja na huduma ya kwanza Afrika Magharibi ya 3.5 G.
Wateja wote wa Zain walipo katika mpango wa malipo kabla na malipo baada wanaweza kupiga na kupokea simu kwa kutumia laini zao za kila siku wakiwa katika nchi yoyote kati ya nchi 16 zinazotunia One Network bila kulipia ghrama za zuru za kimataifa wala gharama za kupokea simu.
Pia wanaweza kuongeza muda wa maongezi kwa kutumia kadi za muda wa maongezi za nyumbani walikotoka au zaidi ya vituo 150,000 Afrika na Mashariki ya kati na kunufaika kwa kupata huduma kama wakazi wa nchi ambayo wametembelea.
"Mteja wa Zain akivuka mpaka na kuingia nchi nyingine anaunganishwa moja kwa moja katika mtandao wa One Network na hahitaji kujisajili wala kulipia ada yoyote. Wateja wanaweza kupiga na kupokea simu na kutuma ujumbe kwa viwanbgo vya nchi waliopo, wanapokea zimu zinazoingia bure katika nchi yoyote kati ya 16 za One Network," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Khaled Muhtadi.
"Huduma ya Zain ya One Network inadhihirisha umahili za Zain katika swala la ubunifu. Huduma ya One Work inapatika katika nchi 16 Afrika na Mashariki ya Kati ambazo ni; Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria, Niger, Chad, Malawi, Gabon, Democratic Republic of the Congo, Congo Brazzaville, Ghana, Burkina Faso Sudan, Jordan, Bahrain, Iraq na Ufalme wa Saudi Arabia," Mkurugenzi Mtendaji wa Zain alisema.
0 comments:
Post a Comment