Mbwana Matumla
MBWANA Matumla 'Golden Boy', amedhihirisha yeye bado wamo baada ya kumpiga kwa pointi Francis Miyeyusho Jumamosi, Januari 17 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Hii inakuwa mara ya pili kwa Mbwana kumpiga bondia huyo, awali akimpiga kwa TKO raundi ya sita. Nani sasa anaweza kujitolea kuzipiga na Mbwana, mbabe wa uzito wa Bantam? Kumbuka Yule Magoma Shaaban wa Tanga alishadundwa hadi akaamua kustaafu. Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona, kwani vijana wapo kwenye ma-gym wanajifua ile mbaya, ni suala la kujitolea tu, ambalo linahitaji moyo.
0 comments:
Post a Comment