Kiungo wa Yanga, Athumani Iddi 'Chuji' (pichani), juzi alifunga bao lake la tatu msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tz Bara.
Chuji aliyefunga mabao mawili kwenye michuano ya Challenge mjini Kampala Uganda, alifunga bao lake la tatu katika Ligi Kuu, kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, wakati timu yake, ikimenyana na Prisons.
Hilo lilikuwa bao pekee lililoiwezesha Yanga kubeba pointi tatu muhimu katika harakati zake za kutetea ubingwa wake.
0 comments:
Post a Comment