Friday, April 11, 2025

    RAIS DK. SAMIA AWAKARIBISHA MAN UNITED KUFUNGUA AKADEMI NCNINI


    RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan leo amekabidhiwa zawadi ya jezi ya klabu ya Manchester United ya England iliyosainiwa na wachezaji wake.
    Rais Samia amekabidhiwa zawadi hiyo na Mmiliki mwenza wa klabu hiyo, Sir Jim Ratcliffe, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. 
    Sir Jim Ratcliffe ameeleza dhamira yake ya kuitumia Manchester United kutangaza utalii wa Tanzania na Rais Dk. Samia pia amempa fursa kuanzisha Vituo vya Mafunzo ya kandanda kwa vijana nchini.


    Pamoja na hayo, Rais Dk. Samia amemkabidhi Sir Jim Ratcliffe zawadi ya picha pamoja na Jezi ya Timu ya Taifa Tanzania, Taifa Stars yenye Ujumbe wa; “Amaizing Tanzania”.
    Dkt. Samia amemshukuru Sir Jim Ratcliffe kupitia Taasisi yake ya Six Rivers ambayo inajishughulika na masuala ya Uhifadhi, kwa namna inavyofanya vizuri katika kudhibiti muingiliano wa wanyamapori na binadamu kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).
    "Nimesikiliza dhamira ya Sir Jim Ratcliffe kuitumia Klabu ya Manchester United kutangaza utalii wa nchi yetu, ambapo pia nimemkaribisha kuanzisha Vituo vya Mafunzo ya Michezo (Sports Academy) hapa nchini,". 
    "Nimepokea na kumshukuru kwa salamu za kheri toka kwa Kocha Ruben Amorim kwa niaba ya wachezaji wa Klabu ya Manchester United, na za Kocha Mstaafu, Sir Alex Ferguson," amesema Rais Dk Samia.
    Kupitia Taasisi yake hiyo ya Six Rivers — Sir Jim Ratcliffe anayemiliki asilimia 28.94 katika klabu ya Manchester United dhidi ya asilimia 71.06 za Malcolm Glazer na Familia yake ameelezea nia yake ya kurejesha hadhi ya Hifadhi ya Taifa ya Selous na kuwa na Wanyama wakubwa katika Hifadhi hiyo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS DK. SAMIA AWAKARIBISHA MAN UNITED KUFUNGUA AKADEMI NCNINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry