Monday, April 07, 2025

    DODOMA JIJI ILIVYOITANDIKA KENGOLD 3-0 JANA UWANJA WA JAMHURI


    WENYEJI, Dodoma Jiji jana waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kengold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
    Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na winga Iddi Bahati Kipagwile kwa penalti dakika ya 43, mshambuliaji Paul Peter Kasunda dakika ya 73 na kiungo Mkongo, Mwana Kibuta David dakika ya 81.
    Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji inafikisha pointi 31 na kusogea nafasi ya saba, wakati Kengold inaendelea kushika katika Ligi Kuu ikibaki na pointi zake 16 baada ya timu hizo zote kucheza mechi 25.
    Ligi Kuu inashirikisha timu 16 na mwisho wa msimu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DODOMA JIJI ILIVYOITANDIKA KENGOLD 3-0 JANA UWANJA WA JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry