TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Kengold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na winga Mgambia, Gibrill Sillah dakika ya 28 na kiungo mshambuliaji, Nassor Saadun Hamoud dakika ya 40.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 51, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi sita na Simba SC ambayo pia ina mechi mbili mkononi na wote wapo nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 61 za mechi 23.
Kwa upande wao Kengold baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 16 baada ya kucheza mechi 24 na wanaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16.
0 comments:
Post a Comment