TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania usiku wa kuamkia leo imechapwa mabao 2-0 na wenyeji, Morocco katika mchezo wa Kundi E kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico.
Mabao ya Simba wa Atlasi yaliyoizamisha Taifa Stars yamefumgwa na beki wa Real Sociedad, Nayef Aguerd dakika ya 51' na kiungo wa Real Madrid, Brahim Díaz kwa Penalti dakika ya 58 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Oujda.
Kwa matokeo hayo, Morocco inafikisha pointi 15 katika mchezo wa tano, ikiendelea kuongoza Kundi E, wakati Tanzania inabaki nafasi ya tatu kwa pointi zake sita ikizidiwa tu wastani wa mabao na Niger baada ya wote kucheza mechi nne.
Timu nyingine kwenye Kundi hilo, Zambia inashika mkia kwa pointi zake Tatu za mechi nne pia.
Timu nyingine mbili zilizopangwa katika Kundi hilo, Eritrea ilijitoa na Kongo - Brazzaville imeenguliwa baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ikiwa tayari imecheza mechi tatu na kufungwa zote.
0 comments:
Post a Comment