KOCHA Hemed Suleiman ‘Morocco’ amemrejesha kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars mshambuliaji Kelvin Pius John wa Aalborg BK ya Denmark kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyeji Morocco Machi 25 Uwanja wa Honor mjini Oujda.
Kuelekea mchezo huo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 zinazoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico — Kocha Morocco hajamjumuisha Nahodha, Mbwana Ally Samatta wa PAOK ya Ugiriki kwa sababu ni majeruhi.
Lakini pia hajawaita makipa wazoefu Aishi Salum Manula wa Simba SC na Metacha Boniphace Mnata wa Singida Black Stars ambao wamepoteza nafasi kwenye klabu zao.
Badala yake amewateua Yakoub Suleiman wa JKT Tanzania, Hussein Masaranga wa Singida Black Stars na Ally Salim wa Simba SC, huku pia
akiendelea kumfumbia macho beki na Nahodha wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto.
Hajamuita pia mfungaji wa bao la Taifa Stars kwenye ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Zambia, Waziri Junior Shentembo anayechezea Al-Minaa ya Iraq kwa sasa.
Katika mechi zake tatu za awali, Taifa Stars imeshinda mbili zote ugenini dhidi ya Niger Novemba 18, mwaka 2023 na Zambia Juni 11 mwaka jana — wakati mchezo mwingine ilifungwa nyumbani 2-0 na Morocco Novemba 21 mwaka 2023.
0 comments:
Post a Comment