TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Big Man FC ya Tanga leo
Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo wa michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB, mabao ya Simba SC yamefungwa na winga Mzambia, Joshua Mutale dakika ya 16 na mshambuliaji Mcameroon, Christian Leonel Ateba Mbida kwa penalti dakika ya 31, wakati bao pekee la Big Man FC limefungwa na Joseph Henock dakika ya 45.
0 comments:
Post a Comment